Habari za Punde

NMB YAWAFUNDA WAZAZI WALEZI NA WALIMU WA SHULE YA MSINGI OYSTERBAY IKIAHIDI SAMANI ZA WALIMU MEZA 40 NA VITI 40

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio, ambaye ni mgeni rasmi katika mafali ya Darasa la saba Shule ya msingi Oysterbay,akimsaidia kumsukuma katika kiti cha kutembelea (wheel chair) mwanafunzi, Harrison Peter, kuelekea katika viwanja vya  sherehe ya maafali ya Darasa la saba yaliyofanyika shuleni hapo ijumaa Sept 20. Kulia ni Meneja wa NMB Tawi la Oysterbay, Subira Kapita, (kushoto mwenye kaundasuti ya kijivu) ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Egidius Mjunangoma. Katika maafali hayo Benki ya NMB iliahidi kutoa msaada wa Viti 40 na Meza 40 za walimu baada ya kusikiliza na kupokea Risala ya wanafunzi wahitimu. 
Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio, mgeni rasmi katika mafali ya Darasa la saba Shule ya msingi Oysterbay,akizungumza wakati wa sherehe ya maafali ya Darasa la Saba yaliyofanyika shuleni hapo ijumaa Sept 20. Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Oysterbay, Subira Kapita, (wa pili kulia) ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Egidius Mjunangoma. Katika maafali hayo Benki ya NMB iliahidi kutoa msaada wa Viti 40 na Meza 40 za walimu baada ya kusikiliza na kupokea Risala ya wanafunzi wahitimu
********************************************
ILI kuharakisha ustawi wa Huduma Jumuishi za Kifedha kwa Jamii, sambamba na kutokomeza mikopo kandamizi ‘kausha damu,’ Benki ya NMB imewataka walimu, wazazi na walezi nchini, kuongeza kasi katika kuwekeza Elimu ya Fedha na Utamaduni wa Kuweka Akiba mioyoni na akilini mwa watoto.
Wito huo umetolewa na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio, wakati wa mahafali ya wanafunzi wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam, alikokuwa mgeni rasmi akimwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki hiyo, Bi. Ruth Zaipuna.
Bw. Urio alisema moja ya changamoto zinazokwamisha ajenda ya kimkakati ya kuongeza idadi ya Watanzania wanaotumia Huduma Jumuishi za Kibenki ni pamoja na ukosefu wa elimu na utamaduni chanya wa kujiwekea akiba ‘saving culture’ kwa watoto ambao ndio taifa la kesho.
“Ndugu wazazi wenzangu, walezi na hata walimu, moja ya changamoto tuliyonayo ni kutokuwa na tabia ya kujiwekea akiba na kwa sababu hatukufunzwa tangu utotoni, imekuwa ngumu kwa sasa kujiwekea akiba na tumefikia hatua, amani ya mioyo yetu ni pale tunapomaliza mishahara yetu kwenye akaunti.
“Sasa hiyo ni changamoto kubwa sana na ndio iliyoifikisha jamii katika ukopaji mikopo kandamizi ambayo hutambulika kama kausha damu, ambayo limekuwa janga kubwa sana hususani kwa kada hii ya walimu. Kwa hiyo nasisitiza tuanze kuwajengea Watoto utamaduni wa kujiwekea akiba.
“NMB tunayo masuluhisho yote yanayohitajika katika kuwakuza watoto chini ya utamaduni huo chanya, tunayo Mtoto Account (chini ya miaka 13), Chipukizi Account (kwa watoto wa miaka 13 hadi 18 na tunayo Mwanachuo Account, ambazo ndio za kuwajenga Watoto,” alisema.
Aidha, Urio alitumia nafasi hiyo kunadi Akaunti za Vikundi, ambazo ni muafaka kwa walimu, vikundi vya kijamii, wajasiriamali, bam ana mama lishe, watoa huduma ya usafiri kwa njia ya pikipiki ‘bodaboda’, sambamba huduma ya mikopo ya Mshiko Fasta hadi Sh, Mil, 1 bila dhamana.
Mbele ya wazazi, walezi na waalikwa zaidi ya 300, na wahitimu 186, Urio aliushukuru uongozi na Bodi ya Shule ya Oysterbay kwa kuitazama NMB kama mshirika sahihi kiasi cha kuipa heshima ya kushiriki mahafali hayo ya nne ya shule hiyo tangu ilipoanza kutumia Mtaala wa Kiingereza.
 Urio alisema kuwa benki yake inajivunia heshima na thamani inayopewa na jamii, na kwa kutambua na kuthamini hilo, kwa mwaka wa 10 mfululizo sasa inatoa asilimia moja ya faida yake baada ya kodi kurejesha kwa jamii (CSR), ili kusaidia utatuzi wa changamoto katika elimu, afya na majanga.
“Tumesikia hapa kupitia risala ya wahitimu, ikitaja changamoto mbalimbali wanazotamani kuona zinapatiwa utatuzi ili kuwawezesha walimu na wanafunzi wanaowaacha kuwa kwenye mazingira rafiki ya ufundishaji na ufundishwaji, kupitia fungu la CSR, NMB inaenda kumaliza baadhi ya hizo hapa hapa.
“Kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB ambaye ameshindwa kuja kutokana na mkwamo wa kimajukumu, naahidi kukabidhi kwa Shule ya Msingi Oysterbay viti 40 na meza 40 kwa ajili ya matumizi ya walimu, ambavyo vimetajwa kama changamoto katika risala,” alifafanua Urio.
Awali akisoma risala ya shule, Mhitimu Eva Henry Nyaki, alisema shule yao iliyoanzishwa mwaka 1952 kwa usajili namba EM 810, ina uhaba wa viti na meza za walimu, kompyuta, mashine za ‘photo copy’ na ‘printer,’ kwa ajili ya kurahisisha uandaaji na uchaapaji wa mitihani na majaribio.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Egidius Mjunangoma, aliishukuru NMB kwa kujitoa kusaidia utatuzi wa changamoto zilizotajwa kwenye risala ya wahitimu na kwamba msaada wa viti 40 na meza 40 kutoka NMB, umekuja wakati muafaka, akiamini vitakuwa chachu ya ufundishaji kwa walimu wake.
Mapema kabisa, Meneja wa NMB Tawi la Oysterbay, Bi, Subira Peter, aliwataka wazazi na waalikwa kuchangamkia huduma mbalimba zinazotolewa na benki yako katika viwanja hivyo ama matawini, ikiwemo Bima ya Afya, Bima ya Elimu kwa Watoto, Bima ya Moto na Bima ya Vyombo vya Ndani.
Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio, mgeni rasmi katika mafali ya Darasa la saba Shule ya msingi Oysterbay,akimkabidhi Cheti cha kuhitimu Darasa la Saba mwanafunzi, Iptisam Ibrahim, wakati wa sherehe ya maafali ya Darasa la Saba yaliyofanyika shuleni hapo ijumaa Sept 20. Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Oysterbay, Subira Kapita, (wa pili kulia) ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Egidius Mjunangoma. Katika maafali hayo Benki ya NMB iliahidi kutoa msaada wa Viti 40 na Meza 40 za walimu baada ya kusikiliza na kupokea Risala ya wanafunzi wahitimu.
Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio, mgeni rasmi katika mafali ya Darasa la saba Shule ya msingi Oysterbay,akimkabidhi Cheti cha kuhitimu Darasa la Saba mwanafunzi, Aisha Kipemba, wakati wa sherehe ya maafali ya Darasa la Saba yaliyofanyika shuleni hapo ijumaa Sept 20. Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Oysterbay, Subira Kapita, (wa pili kulia) ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Egidius Mjunangoma. Katika maafali hayo Benki ya NMB iliahidi kutoa msaada wa Viti 40 na Meza 40 za walimu baada ya kusikiliza na kupokea Risala ya wanafunzi wahitimu. 
Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio, mgeni rasmi katika mafali ya Darasa la saba Shule ya msingi Oysterbay, akipokea Risala kutoka kwa mhitimu wa darasa la saba, Eva Henry, wakati wa sherehe ya maafali hayo yaliyofanyika shuleni hapo ijumaa Sept 20. Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Oysterbay, Subira Kapita, (wa pili kulia) ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Egidius Mjunangoma. Katika maafali hayo Benki ya NMB iliahidi kutoa msaada wa Viti 40 na Meza 40 za walimu baada ya kusikiliza na kupokea Risala ya wanafunzi hao wahitimu. 
 Meneja wa NMB Tawi la Oysterbay, Subira Kapita, akizungumza kufaanua baadhi ya huduma zitolewazo na Benki hiyo, kama kufungua akaunti za watoto na nyinginezo wakati wa sherehe ya maafali hayo yaliyofanyika shuleni hapo ijumaa Sept 20. Kushoto kwake ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seko Urio, (wa tatu kutoka kushoto) ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Egidius Mjunangoma. Katika maafali hayo Benki ya NMB iliahidi kutoa msaada wa Viti 40 na Meza 40 za walimu baada ya kusikiliza na kupokea Risala ya wanafunzi hao wahitimu. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.