Habari za Punde

SUFIANIMAFOTO INAWALETEA KUMBUKUMBU YA MATUKIO YA MAPOROMOKO SAME

Huko tulikotoka jamani hapafai hata kusimulia jamani................Sufiaimafoto,(kusoto) akiwa na rafiki yake Maregesi Paul, hapa ni baada ya kushuka kutoka milima ya Mamba Miamba, Kijiji cha Goha ambako yalitokea maafa yaliyosababisha vifi vya watu 24, hapa ni Same mjini. Picha Zote na (SPM)

Mbele ni gari alilotumia Sufianimafoto likipandisha milimani, na picha ya chini likiendelea kupanda milima hiyo iliyofanya safari hiyo ya kupanda mlima kuwa na masaa matatu na nusu.

Bora tufike huwezi jua......................................
Gari aina ya Fuso lenye namba za usajiri T106 AJT likiwa limejaza abiria na mizigo likitoka maeneo ya Vijiji vya Gonja Mpirani, kuelekea Gonja Mahole katika Mnada unaofanyika kila siku ya Alhamisi, bila kujali hali ya barabara hiyo iliyo mbovu kupita kiasi. Hii moja kati ya hali ngumu ya usafiri kwa wakazi wa Vijiji vya Gonja na milima ya Mamba Miamba, hapa wakiwa wamejazana kwenye roli kuelekea maeneo ya mjini ambako wao huita Gulioni.


Moja ya kati ya Nyumba zilizojengwa pembezoni mwa Mto Chafuwe, inavyoonekana ikiwa na nyufa kufuatia mvua za mfululizo zilizonyesha Wiala ya Same hivi karibuni. Nyumba ya nyumba hiyo ni maji ya Mto Chafuwe yanayotiririka kutoka kwenye Msitu wa Shengena.

Mtoto ambaye hakuweza kufahamika jina lake wa kijiji cha Kisiwani, akiwa kifua wazi nje ya nyumba yao wakati hali ya hewa ikiwa ni ya baridi kama alivyokutwa na mpiga Sufianimafoto hivi karibuni.

Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, David Mathayo, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Goha, wakati wa Misa ya kuwaombea marehemu.

Wakazi wa Kijiji cha Goha wakibeba moja ya jeneza kuweka mahala palipoandaliwa maalum kwa ajili ya kuendesha Misa ya kuwaombea marehemu.

Baadhi ya waombolezaji wakiwa eneo la tukio wakisubiri misa ya kuwaombea marehemu. waliokufa katika maporomoko yaliyotokana na mvua iliyoangusha mawe ya mlima na kufunika numba takriban 8 mahala hapo.

Haya ni baadhi ya maji yanayoporomoka kutoka milimani yakipita maeneo ya makazi ya watu waishio Kijiji cha Goha.

Hivi ndivyo linavyoonekana eneo lililofunikwa, hapa ni eneo lililokuwa na nyumba kadhaa za wakazi wa Goha.

Waombolezaji wa Kijiji cha Goha wakisubiri Misa ya kuwaombea marehemu.

Wakiwa ni wenye huzuni kubwa kwa kupotelewa na ndugu, jamaa na marafiki zao, mikono ikiwa shavuni, kila mmoja akiomba kwa imani yake kuwaombea marehemu.
Badhi ya Majeneza ya marehemu hao yakiwa pamoja kabla ya misa na kuzikwa katika makabri yaliyoandaliwa katika eneo moja.

Wakazi wa Kijiji cha Goha wakimuonyesha Mpiga Sufianimafoto, (katikati) baadhi ya maeneo yaliyokuwa na nyumba ambayo yamefunikwa kwa udongo na mawe baada ya maporomoko hayo.
Sehemu ya mlima iliyomomonyoka huku maji yakiendelea kushuka kwa kasi.


Vijana watatu walionusurika kwenye maporomoko hayo wakipongezana.

Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula, David Mathayo, akitembezwa na baadhi ya viongozi wa Kijiji hicho kuonyeshwa maeneo yaliyoathirika kwa maporomoko.

Hii ni baadhi ya mifugo iliyosombwa na mafuriko hayo.

Hili ndilo eneo lililokuwa na nyumba hizo, likiwa mithili ya shamba lililoandaliwa tayari kwa kupanda mazao.
Askari Polisi na Mgambo wa Wilaya ya Same wekiendelea na zoezi la kutafuta miili ya marehemu waliopotea.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Goha wakitafuta miili iliyopotea kwenye Mto Chafuwe.

Mmoja kati ya wakazi wa Kijiji hicho akilia kwa uchungu.

Mtoto wa Kijiji cha Mamba Kata ya Miamba, akiwa na vidumu vya maji akitoka kutafuta maji katika milima ya vijiji hivyo.
Wanakijiji wakibeba mwili wa mmoja wa marehemu aliyepatikana kwenye mto Chafuwe.

Wanakijiji wa Mamba Miamba, wakisubiri usafiri huku wakivaa nguo kituoni hapo haikujulikana sababu za wanakijiji hao kuvalia nguo kituoni hapo.

























No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.