BAADA ya kimya cha muda mrefu, mwimbaji wa muziki wa dansi Ramadhan Masanja 'Banza Stone' ambaye hivi karibuni alikuwa akisumbuliwa na maradhi, anatarajia kuipa shavu bendi ya Bwagamoyo International wakati wa sikukuu ya Krismasi.
Akizungumza na SPM, kwa njia ya simu kutoka Mkoani Tanga ambako bendi hiyo imeweka Kambi yake, kwa ajili ya kuandaa albamu yao ya kwanza, Mkurugenzi wa bendi hiyo Muumin Mwinjuma alisema kuwa Bwagamoyo International inatarajia kuahirisha kambi ya mazoezi ili kuweza kutoa burudani wakati wa shehereke za sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya katika baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa ya Shinyanga, Mwanza na Mara.
Alisema kuwa wamemualika Banza Stone katika maonyesho yao ya sikukuu hizo na ameshajiunganao kambini kwa ajili ya kufanya mazoezi ya baadhi ya nyimbo zao ambazo atapanda jukwaani na kuimba sambamba na wanamuziki wa bendi hiyo.
"Banza amesharipoti kambini na tayari ameshaanza mazoezi ya pamoja na wanamuziki wa Bwagamoyo International” alisema Kocha wa Dunia aliyepania kurudisha heshima yake kama enzi za Mkulima kala Mbegu. Aidha alisema kuwa Banza Stone ni mwanamuziki huru kwa hivi sasa ambaye hajaamua kujiunga na bendi yeyote, hivyo ameona ni bora kuwa naye kwa kipindi hiki cha sikukuu ili kuwasalimia mashabiki wake wa mikoani ambao wanatamani kumuona na kumsikia akiimba baada ya kuwa kimya kwa kipindi kirefu akisumbuliwa na maradhi.
Kocha wa Dunia alitaja baadhi ya mikoa ambayo watafanya maonyesho kuwa ni Manyoni mkoani Singida wakati ikielekea mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambapo onyesho la pili litafanyika Nzega mkoani Tabora.
"Onyesho jingine litakuwa ni la mkesha wa Krismasi ambalo litafanyika mjini Shinyanga na katika maonyesho hayo ya awali tutakuwa bila Banza Stone ambaye ataungana nasi siku ya Krismasi mjini Kahama," alisema.
Alisema kuwa baada ya onyesho hilo la sikukuu ya Krismasi wataelekea mjini Musoma mkoani Mara kuendelea na ziara yao hadi mwaka mpya wa 2010 na kisha watarejea kambini kuendelea na mazoezi ya kukamilisha albam yao.
Alizitaja baadhi ya nyimbo za bendi hiyo zilizokwishakamilika kuwa ni pamoja na Nafsi Haina Urithi, Baba wa Kambo, Udugu wa Mashaka, Cute Baby, Natafuta Mume na Nani Kama Mama ambazo zote zitapigwa katika maonyesho hayo.
Bendi hiyo inayotumia mtindo mpya wa ‘Gusa Unase’ ilijiimarisha hivi karibuni kwa kupata wanamuziki wapya, waimbaji, wapiga vyombo na wanenguaji ambao tayari wameshaonyesha makali yao kwenye nyimbo hizo zinazoandaliwa kwa ajili kurekodiwa.

No comments:
Post a Comment