
Maharusi Saleh Mohamed, akiwa na mkewe, Amina mara baada ya kufunga ndoa nyumbani kwa mama mzazi wa Amina Ilala, hivi karibuni.

Saleh, akiingia ukumbini na mkewe wakati wa sherehe ya ndoa yao.
"Duh! siamini babake kama nimeweza kukamilisha na kufanikisha wacha nifurahi..."
Saleh Mohamed akipagawa kwa furaha mara baada ya kuingia ukumbini, wakati wa sherehe ya harusi yake.

Ni furaha ilioje leo jamani tuginganishe grasi kwa furaha zetu.

Maharusi wakiwa na furaha ya kutosha, meno thelathinanje yote mbili.

Hawa ni baadhi ya wafanyakazi wa Free Media, wakipita kugonganisha grasi na maharusi.
"Kunywa yoooote usibakize hata kidogo......"
Saleh Mohamed, akimnywesha Champaign, mkewe Amina.

Saleh na mkewe na wasimamizi wao wakinyweshana naniliu.....

Hii ya kwetu ole wenu muige,........
"Haya tunyweshane wote sasa kwa raha zetu..." 
Hii ni furaha tuuuuu, wakiendelea kunyweshana kama walivyoagizwa na mwongozaji wa sherehe (MC) hadi iishe.

Saleh na Mkewe, Amina, wakikata keki kwa pamoja kuashiri kuwa ni mwili mmoja baada ya kuhalalisha mambo flani siku hiyo mchana.
"Tumeshakuwa mwili mmoja na kitu kimoja, haina shida we nilishe utakavyo" 
Saleh na mkewe wakilishana keki kama ndege tunduni,

Wakipozi jukwaani

Hii ni mindoko ya blues, si kama wamelala na kujifunika neti la hasha, ni mapozi tuuuuu.

Baadhi ya wageni waalikwa wakisebeneka sambamba na maharusi.

Hii ni miondoko ya kuelekea kutoa zawadi, si wengine ni baadhi ya wafanyakazi wa Free Media, wengine utadhani walitoa mchngo mkubwa kuliko wenzao kwani furaha ilipitiliza kila sebene wao twende.


Saleh, akisebeneka na bibi zake kwa furaha wakati wa zawadi.

Si mdumange huu, ni Sebene tena la haja.....

Utazani anacheza miondoko ya Makirikiri kutoka Afrika ya Kusini vileee.

Ni furaha tuuuuuuuuuu........


Wafanyakazi wa Free Media, wakitoa mkono wa pongezi kwa miondoko ya sebene.

Saleh Mohamed na Mkewe, Amina wakipiga picha ya kumbukumbu na wafanyakazi wenzake na Saleh.

Mwakilishi wa wafanyakazi wenzake kutoka Free Media, Swaum (mwenye mic), akizungumza neno kwa niaba ya ofisi yao, wakti wa muda wa kutoa zawadi na mkono wa pongezi.
No comments:
Post a Comment