Menu

Monday, December 28, 2009

*YANGA ILIVYOMCHINJA PAKA KWA WEMBE KOMBE LA TUSKER

Ushindi Mtamu bwana weeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!Wachezaji wa Yanga, wakimbeba Kocha wao wakati wakishangilia ushindi mara baada ya kumalizika kwa mtanange baina yao na Sofapaka, ambapo Yanga ilishinda katika Fainali hiyo kwa kuwachapa 2-1. Picha ZOte na (SPM)



Na bado mtanitambua kwenye Ligi huu ni mwanzo na mfano tuuuuuu.

Jerry Tegete, akiwa na kikombe chake cha Mfungaji Bora wa michuano ya Kombe la Tusker, mara baada ya kukabidhiwa.


Oya msinitolee mimacho me nimebehili kombe, hata we msomaji usinitolee macho nalipa eeeeee!


Mrembo akipozi na Kombe la Tusker wakati wa muda wa kukabidhi zawadi wa washiriki wa michuano hiyo.

Hata mfanyeje vymbani kwenu hatuingng'oooooo, tutavalia hapa hapa kama mlishaloga mtajiju.


Wachezaji wa Timu ya Sofapaka, wakivalia kwenye Bechi badala ya kuingia vyumbani kwa madai kwamba wanaogopa upupu, hata timu hii inayomilikiwa na Kanisa huko kwao inaamimambo haya badala ya kumuaimini yule naniliu tu awalinde?????

Duh! mbona dakika haziendi? jamaa wanatuhemea golini kwetu kila dakika.....


Viongoizi wa Sofapaka, wakiangalia muda wakati mchezo huo ukiendelea, hawaamini macho yao kwa kile wanachokiona jinsi wanavyoshambuliwa.

Oyaa usinitolee mimacho, hunitishi kiivyo, alaaa, kama unahasira si ukampige Ngassa, aliyewatesa kwa michenga ya maudhi, au unatufananisha nini me si Ngassa tunafanana ufupi tu.



Hivi ndivyo ilivyokuwa washikaji, me sikupigwa kama ilivyotangazwa hili jamaa lilikuwa likizuia tusipige picha kipa wao wakati alipokuwa akiarestiwa na maafande alipokuwa akijaribu kumpiga refa

Mkifika hapa pigeni, na hawa jamaa msiwaruhusu kufika hapa watatumaliza wanaonekana wanakuja mno....
Kocha wa Sofapaka akiwaelekeza wachezaji wake kwa kutumia ubao wakati wa muda wa mapumziko, ili kulinda gori lao walilopata kwa njia ya adhabu ndogo kipindi cha kwanza.


Kipa wa Sofapaka, akioa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni kwake.

Beki wa Sofapaka, Edgar Ochieng (kulia) akimhadaa Mrisho Ngassa.



Wachezaji wa Yanga na wa Sofapaka, wakibishana, wakati wakimtaka kipa wa Sofapaka kuondoa mkoba uliokuwa na grovs, unaoonekana ndani ya nyavu waliouzania kuwa ni tunguli lililowekwa na kipa huyo ili asifungike kirahisi.

We tulia weweeeee, unalia nini hako kateke kadogo tu we unalia hapa tupo 18 yenu usidhani uatapata penati.....


Athuman Idd 'Chuji) (kulia) akicheza rafu baada ya beki wa Sofapaka kuondosha mpira mbele yake.

Beki wa Yanga, Amir Maftah (kulia) akimtoka beki wa Sofapaka, Kamadi Michael, wakati wa mchezo huo.

Hawa ni baadhi tu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es salaam.

Jerry Tegete (kulia) akimtoka beki wa Sofapaka, Tumba Kilonzo.
Tulia hivyo hivyoooooo!

Kijana aliyedaiwa kumkwapulia simu jamaa mmoja wakati wakiwa kwenye msonamano wa watu kibwena, uwanjani hapo.
Nenda kawaue mdogo wangu.............................

Mrisho Ngassa (Kushoto) kiwatoka mabeki wa Sofapaka baada ya mpira kuwapita wote waliporuka kupiga kichwa na AdKassim (kualia) na kuandika bao la pili na la ushindi.

Hata ni we ni Mkei mwenzangu lakini hapa nimekuja kazini wacha nifanye kazi kwanza we tulia tuuu, me ndo Ambani tutaonana nyumbani mazee...

Boniface ambani akichuana na kipa wa Sofapaka na kuandika bao la kwanza la Yanga.
Si mnanitaka ? hivi ndivyo vitu vyangu kwanza kazi nikija kwenu tusahau haya ok?
Mrisho Ngassa, akifunga bao la pili na la ushindi kwa timu yake ya Yanga, hili ndilo gori la ushindi.

Aisee rudini uwanjani tukamalizie dakika zilizobaki hamsikii nitawapa kadi nyekundu wote nyie..
Refa wa mchezo huo akiwaamuru wachezaji wa Yanga kurudi uwanjani wakati walipokuwa wakishangilia bao lao la pili.
Sasa ile ndo nini Kipa anataka kumpiga Refa kwani ndo aliewafunga? Si wampige Ngassa? ona ona......

Kocha wa Yanga (kulia) akiwashangaa wachezaji wa Sofapaka waliokuwa wakitaka kumpiga Refa baada ya mchezo huo kumalizika.

Bora mtulinde jamani hawa jamaa utazani ni mungiki! wanahasira haooooooooo!

Askari Polisi wakiwasindikiza waamuzi kutoka nje ya uwanja mara baada ya mchezo huo kumalizika, wakati walipokuwa wakizongwa na wachezaji wa Sofapaka.


Wachezaji wa Yanga wakishangilia kwa staili yao babakeeee.

Hili ndilo Kombe la Tusker likisubiri kukabidhiwa kwa mshindi.

Nyie si mnajifanya mamungiki fanyeni hizo fujo zenu muone tunavyowaogesha maji ya kuwasha.
Gari la maji ya kuwasha la Polisi likianza tisha nyau mara baada ya kuona vurugu zinaanza uwanjani hapo.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia, kwa staili ya mazoezi.
Hureeeeeeeeee, mapesa hayooooo, haya ndiyo matunda ya Samba niliyokujanayo.

Kocha wa Yanga (kulia) na Nahodha wa Yanga. Abdi Kassim, wakipokea hundi ya sh. milioni 40, kutoka kwa Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika.

Wachezaji wa Yanga wakifurahia ushindi wakiwa na Kombe lao mara baada ya kukabidhiwa.

Kocha wa Yanga (kulia) akishangilia sambamba na wachezaji wake baada ya kukabidhiwa kombe lao la michuano ya Tusker.

Askari Pilosi wakimdhibiti kijana aliyedaiwa kupora simu katikati ya msongamano wa watu.






























































No comments:

Post a Comment