"Oyaa! Masela ndo mie jamani mmeniona? niko vile vile sibadiliki au vipi masela..."
Askari wa usalama akimlinda Didier Drogba, mara baada ya mchezo kumalizika, hivi ndivyo jamaa alivyokuwa akilindwa, imeelezwa eti Chama lake limemtumia jaa ulinzi kutoka huko huko majuu, ukiongeza na wa hapa ebwanae usipime asogei mtu.
Mashabiki wa Soka wakimshangilia Didier, wakati akitoka uwanjani.
Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali, wakimhoji Colo Toure, mara baada ya mchezo kumalizika.
Colo Toure (kushoto) na Didier Drogba, wakipiga picha ya kumbukumbu na wachezaji wa timu ya Amavubi, baada ya mchezo kumalizika.
Beki wa Rwanda, Didier Kouin Kapet (kushoto) akiruka kuwania mpira na Kipa wa Ivory Coast, Barry Boubakar, wakati wa mchezo wao wa kirafiki. Ivory Coast ilishinda 2-0.
"Duh! kumbe kupiga picha raha namna hii sasa peni naweka chini rasmi, Drogba namuona hapa mbele kabisaaaa"!!!!!
Huyu ni Mwandishi na Mhariri wa gazeti na Michezo la Champion, akiwajibika wakati wa mchezo huo wa kirafiki, hatumwi mtoto Sokoni, sijui aliona viajana wake wanampelekea Drogba aliye Auto Focus akaamua kuingia mzigoni mwenyewe?, Aminia babakeeeeee
Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati wanaume wameamua kusaka gori, dakika zote wako langoni mwa Amavubi, hii ni moja kati ya hatari zilizookolewa na mabeki na kipa wa Amavubi, Sifa za pekee zinamstahili Kipa huyo kwa kuokoa michomo kibao na ya ukweli kwani yalikuwa ni mashuti ya nguvu na mengine yaliyokuwa yakigonga mwamba na kutoa sauti iliyosikika uwanja mzima, hapa ni beki akiokoa hatari hiyo.
Jamaa baada ya kuzidiwa na spidi ya hatari hatimaye walilegea na kuruhusu magoli 2 ya fasta na yote yakitiwa kimiani kwa vichwa.
No comments:
Post a Comment