Habari za Punde

*STARS WAJIKAKAMUA, KWA IVORY COAST, WAONYESHA UWEZO, DROGBA ATUPIA KIMOJA

"Hili ndilo Soka la mamtoni bwana mdogo we tulia tu usije aibika bureeee"Mshambulia jiwa Timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba (kushoto) akiruka kumiliki mpira mbele ya Beki wa Taifa Stars, Juma Jabu, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliochezwa kwnye Uwanja wa Taifa
Dar es Salaam leo jioni. Ivory Coast ilishinda 1-0. Picha na (SPM)
"Hapa hupiti kirahisi wewe, hata kama we ni wa kwenye Kiooo Alaaaah!"
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba (kushoto) akichuana na beki wa Taifa Stars, Nadir Haroub, wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Ivory Coast ilishinda 1-0.

Mrisho Ngassa, wa Taifa Stars, (kushoto) akibanwa na beki wa Ivory Coast na kukosa bao la wazi katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Walinzi wakiwa wamezuia gari la waandishi wa habari wa Televisheni ya Taifa TBC1, ili lisiingie ndani ya Uwanja wa Taifa, wakidai waonyeshwe kadi maalum za kuingilia ndani japo waandishi hao waliwaonyesha vitambulisho vyao vya kazi, lakini bado jamaa walikomaa na kufunga mageti kama wanavyoonekana.
Ebwana eeeh! kumbe ndo wewe mwenye vijineno vile duh!....au Fata....
Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, George Mkuchika (wapili kulia) Naibu wake, Joel Bendera, (katikati) wakifurahia jambo na Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mrisho Mpoto wakati wakiingia kwenye Uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Ivory Coast na Taifa Stars jana.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.