Habari za Punde

*ANDAZI LAZUA KIZAAZAA BENKI YA NMB, DAR

Andazi lazua kizaazaa benki ya NMB Makao Makuu Dar

Na Mwandishi wetu
ANDAZI lililosahaulika kwenye mashine ya kupashia chakula moto (Microwave), jana mida ya saa tano na dakika kadhaa lilileta patashika kwa wafanyakazi na wateja waliokuwa wamejazana ndani ya benki ya NMB, Makao Makuu iliyopo Mtaa wa Azikiwe jijini Dar es Salaam, baada ya mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo kuacha andazi alilokuwa akipasha moto katika mashine ya kupashia chakula moto ‘ Micro Wave’ na kupata moto hadi kuwaka na kulipuka mithili ya bomu huku sahani iliyokuwa na andazi hilo ikitoa mlio mkubwa na wakutisha.
Baada ya mlio huo ilibonyezwa kengere ya alam kuashiria hatari, na hivyo kuwafanya wafanyakazi wa benki hiyo na wateja waliokuwamo, kuhaha na kumenyana katika milango wakigombea kupita ili kujinusulu maisha yao na kile walichozani jingo hilo lingeweza kuwaka kufuatia mlio huo.
Ndani ya jingo hilo pia alionekana mlemavu ambaye alikuwa akijitahidi kuhangaika kukimbia na kushuka ngazi kwa kasi bila kuwa na msaada huku kila mmoja akikimbia kunusulu maisha yake bila kumjali, jambo ambalo inabidi kutiliwa mkazi wakati wa ujenzi wa majengo mengine makubwa yanayoendelea kujengwa ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam.
Aidha chanzo cha habari hizi kilidai kuwa mtu huyo aliyekuwa akipasha moto andazi hilo baada ya kusikia mlio huo naye pia alitimua mbio huku akiwa na wa kwanza kutoka nje ya jengo hilo bila kujua kilichotokea.
Iliwachukua kiasi cha dakika 20 huku walinzi wa jingo hilo wakihaha kutafuta chanzo na kufanikiwa kuizima ‘Wave’ hiyo na kuzima alama kasha kutoa taarifa ili wafanyakazi wa benki hiyo waweze kurejena na kuendelea na kazi, jamboa ambalo pia lilileta kizaa zaa kingine baada ya wateja wa benki hiyo lukuki walioanza kutimua mbio ili kuwahi nafasi zao katika foleni ili kuweza kupata huduma.

Baadhi ya wafanyakazi na wateja wa benki hiyo wakiwa nje na wengine wakiendelea kutoka nje ya benki hiyo, baada ya kupigwa alma ya kuashiria hatari.

Wengine wakiwa hawachezi mbali ili kusubiri kuisha kwa hali ya hatari waweze kuwahi foleni zao ili kuendelea kupata huduma.

Ndivyo hali halisi ilivyokuwa, ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakiwa nje.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.