Habari za Punde

*IGP AFANYA MABADILIKO KWA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la
Polisi-Dodoma


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, amefanya mabadiliko madogo katika safu ya Makamanda wa Polisi wa mikoa na kumteua Kamanda mpya wa Polisi wa mkoa wa Temeke katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi ACP Abdallah Mssika, amesema leo mjini Dodoma kuwa, katika mabadiliko hayo IGP Mwema amemteua Kamishna Msaidi wa Polisi ACP David Missime, kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kuwa
Kamanda mpya wa mkoa wa Kipolisi Temeke.
Amesema Kamanda wa zamani wa Mkoa wa Temeke ACP Liberatus Sabas, amehamishiwa mkoani Tanga kuchukua nafasi ya Kamanda Simon Sirro anayehamishiwa mkoa wa Mwanza.
Amesema Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi ACP Jamali Rwambow, yeye anahamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Jijini Dar es Salaam Kuimarisha safu ya makachero katika ofisi hiyo.
Tofauti na ilivyoandikwa katika Gazeti moja la Kiswahili la leo Februari 21, Kamanda Mssika amesema kuwa uhamisho huo ni wa kawaida kama ilivyo kwa Makamanda wengine wanapohamishiwa katika mikoa ama maeneo mengine kiutendaji na kuongeza kuwa uhamisho huo unaanza kutekelezwa mara moja.
Wakati huo huo, Makamu wa Rais Dk. Mohammed Shein, leo amemwakilisha Rais Jakaya Kikwete, katika ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi uliofanyika kwenye ukumbi wa Bunge wa Pius wa Msekwa, mjini Dodoma.
Mkuu wa Jeshila Polisi nchini Inspektaq Jenerali Saidi Mwema, alisema kuwa tayari Makamishna na Kamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi, wameshawasili mjini
Dodoma kwa ajili ya mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.