Aliyekaimu nafasi ya Mwamuzi wa akiba katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya Simba na Zesco ya zambi, ASP Jonas Mahanga, ambaye pia ni msimamizi wa usalama katika Uwanja huo, akionyesha kibao cha matangazo wakati akifanya mabadiliko ya mchezaji wa Simba, Ramadhan Chombo. Huyu jama hii si kazi yake ila alifanya hivyo kuokoa jahazi lililokuwa likielekea kuzama.
Mchezaji wa Simba, Uhuru Selemani (kushoto) akichezea mpira mbele ya beki wa Zesco, wakati wa mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa uhuru Dar es Salaam leo jioni. Simba ilishinda 4-1.
Uhuru Selemani, akichanja mbuga, kuwatoka mabeki wa Zesco.
Mshambuliaji wa Simba, Kelvin Chale, akiruka kumkwepa kipa wa Zesco, wakati wa mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam leo jioni. Simba ilishinda 4-1.
Na Sufianimafoto Reporter
KUTOKANA na utaratibu na maandalizi mabovu ya mchezo wa Kimataifa wa
Kirafiki kati ya Simba ya jijini Dar es Salaam na Zesco ya Zambia,
halimanusura mchezo huo usichezwe kutokana na waamuzi wa mtanange huo
kugoma kuingia uwanjani kwa kile kilichodaiwa kupewa posho tofauti na
makubaliano.
Mchezo huo ulianza Saa 11: 05, badala ya saa 10:30 jioni, huku tayari
baadhi ya mashabiki wakionyesha kukata tamaa kuwepo na mchezo huo na
wengine wakianza kupiga kelele kurejeshewa kiingilio chao.
Aidha imeelezwa kuwa makubaliano ya awali kati wa waratibu wa mchezo
huo na waamuzi hao, ilikuwa kila ni waamuzi kulipwa Sh. 80, 000,lakini
walikuta ni tofauti huku wakiwa wameandaliwa Sh 50,000, jambo
lililowafanya kuingia mitini huku wengine wakionekana jukwaani na
mavazi ya disco.
Kutokana na kusuasua kwa maandalizi yote uwanjani hapo, walionekana
waamuzi waliochezesha mchezo huo katika vyumba vya wachezaji wa simba
wakiazima viatu ili kuingia uwanjani kuchezesha mchezo huo.
Baada ya kupatikana muafaka waamuzi hao waliingia uwanjani wakiandamana
na timu zote mbili, huku mchezo huo ukiwa hauna mwamuzi wa akiba.
Kwa tukio hilo la mchezo kukosa Mwamuzi wa akiba, jukumu la kuokoa
jahazi hilo lilichukuliwa na Kamanda Mkuu wa askri wanaosimamia
shughuli za Uwanjani, ACP Jonas Mahanga, aliyekuwa akifanya mabadiliko
ya wachezaji na shughuli zote zinazofanywa na mwamuzi wa akiba, na
kuwafanya mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo kuangua kicheko cha
kejeli.

No comments:
Post a Comment