Gari hilo likiondolewa mtaroni.
Roli la mafuta lenyr namba za usajiri T 189 ABP, likiwa limelalia daladala lenye namza za usajiri T 615 AJW, baada ya roli hilo kugongana uso kwa uso na ahice hiyo na kuiburuza hadi mtaroni, ambapo abiria wote wanaokadiliwa kuwa 10, waliokuwamo katika Hice hiyo walifariki papo hapo katika ajali hiyo iliyotokea leo alfajiri eneo la Kibamba Darajani nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Askari Polisi na Raia, wakimsaidia kijana aliyetambulika kwa jina la Fredy Nicodemasi, aliyeingia mtaroni ili kutafuta mwili wa mama yake mzazi baada ya kupata taarifa za ajali hiyo huku akiwapita waopoaji hao akiwa kama aliyechanganyikiwa.
Gari la kubeba vitu vizito la Kampuni ya BMK, likiondo roli hilo mtaroni ili kuopoa abiria waliokuwa wamebanwa chini ya magari hayo.
Baadhi ya wakazi wa maeneo ya Kibamba, wakiwa eneo la tukio kushuhudia zoezi la uopoaji wa maiti waliokufa katika ajali hiyo, ambapo baadhi yaowaliweza kutambuliwa na raia hao.
Raia, wakimsaidia kijana aliyetambulika kwa jina la Fredy Nicodemasi, aliyeingia mtaroni ili kutafuta mwili wa mama yake mzazi baada ya kupata taarifa za ajali hiyo huku akiwapita waopoaji hao akiwa kama aliyechanganyikiwa.
Gari la kubeba vitu vizito la Kampuni ya BMK, likiondo roli hilo mtaroni ili kuopoa abiria waliokuwa wamebanwa chini ya magari hayo.
"Masikini Mume wangu jamaniiiiii"
Mjane, aliyejulikana kwa jina la Shani Nustafa, ambaye mumewe ni miongoni mwa waliokuwamo kwenye ajali hiyo, akilia kwa uchungu baada ya kufika kwenye eneo la tukio na kuona kitambulisho cha mumewe.
Askari na raia wakishirikiana kuopoa miili ya abiria walionasa kwenye Hice hiyo.
Na Sufianimafoto, Kibamba
AJALI ya kutisha iliyotokea Kibamba darajani leo alfajiti, imekuwa ni ajali kubwa nay a kutisha tangu kuanza kwa mwaka huu ambapo watu waliofika eneo la tukio walijikuta wakiangua vilio na kushikwa na simanzi uhalisia wa ajali hiyo.
Vipande vya miili hiyo zaidi ya watu 8 vilikuwa vikikusanywa na polisi, askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji na baadhi ya wananchi waliojitoea, kutoka kwenye mabaki ya daladala yenye namba T 615 AJW aina ya Toyota Hiace, inayofanya safari zake kati ya Mlandizi na Dar es Salaam, ambayo ilifumulia na kulaliwa na gari aina ya Veco lililokuwa limebeba mafuta ya taa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ajali hiyo ilisababishwa na dereva wa lori lenye namba T 189 ABP lililokuwa na trela lenye namba 192 linalomilikiwa na Mahamoud Mohamed, ambaye inadaiwa alikuwa katika mwendo kasi uliosababisha ahame upande wake na kuifuata daladala kisha kuigonga na kuiburuza hadi kuibamiza kwenye kingo zaa mtaro wa barabara hiyo na kuigandamiza.
Katika tukio hilo, kijana aliyejulikana kwa jina la Fred Nicodemus alitia simanzi zaidi baada ya kuangua kilio cha uchungu, alipobaini kuwa mama yake aliyeitwa Esther Paul ambaye alikuwa ni mjamzito, naye ni miongoni mwa wanawake watatu waliokufa katika ajali hiyo.
Mwili wa mwanamke huyo ulitolewa ukiwa umepasuka tumbo na kusababisha kiumbe kuning’inia, na wakati kijana huyo akilia alikuwa akitamka kwa uchungu; “mama ulikataa kupanda gari la familia kumbe safari yako imeishia hapa.” Kijana huyo alisaidiwa kuondolewa katika eneo hilo na polisi ambao walimkabidhi kwa jamaa zake.
Naye Shani Mustafa, aliangua kilio baada ya kuuona mwili wa mume wake ambao ndiyo pekee uliotoka ukiwa na viungo kamili (haukukatika vipande) ukiwa umelala chini kabisa ya mtaro, akionekana kana kwamba alijaribu kujinasua lakini alishindwa na kupoteza uhai wake papo hapo.
“Jamani mume wangu huyo mume wangu! Nimemtambua wakati anaondoka alivaa hivi kweli umekufa umeniacha, hapana! Naomba angalieni ana kitambulisho chake nione kwanza,” alilia kwa uchungu mwanamke huyo.
Kitambulisho hicho kilipotolewa alitambuliwa kuwa kweli ni mumewe anayeitwa Abutwalib Twahibu, Msimamizi katika kampuni ya Busecom, iliyopo katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mwanamke huyo aliendelea kulia huku akieleza kwamba wakati mume wake anaondoka, aliongozana na dada yake, lakini alishindwa kumtaja jina kwani alikuwa akilia kwa uchungu, na kuishiwa nguvu, na jirani zake walifika na kumsaidia kuondoka naye katika eneo hilo.
Naye Mzee Husen Salehe alieleza kupoteza mtoto wake katika ajali hiyo, ambaye alimtaja kuwa ni Shukuru Huseni (27) ambaye ni maarufu kwa jina la Bwetu, kondakta katika moja ya daladala zifanyazo safari zake jiji Dar es Salaam.
“Mwanangu alikuwa ni kondakta nilikuwa naishi naye, aliamka alfajiri ili kwenda kuamsha gari anayoifanyia kazi, siyo hii aliyopata nayo ajali, nafikiri alipanda ili kufuata gari lake, lakini amekumbwa na mauti, nimeshamtambua ndiyo mwenyewe wala hakuna shaka nimeshampoteza,” alisema mzee huyo kwa uchungu.
Katika hali iliyoonyesha kuchanganyikiwa, mzee huyo ambaye anaonekana kuwa na umri wa kati ya miaka 60 na 65, alijieleza kwamba ana umri wa miaka 40, na kwamba taarifa za ajali ya kijana wake alizipata baada ya dereva wa gari alilokuwa akilifuata kufika nyumbani kwao kumchukua, lakini hakumkuta ndipo wakajulishwa kuna ajali ambayo imetokea na kwamba walifika hapo kumtafuta ndipo mzee huyo akamtambua.
Huku kukiwa na msongamano mkubwa wa magari na wananchi waliokuwa wamezunguka pande zote za eneo la ajali, wengi walionekana wakiwa wametawaliwa na huzuni, majonzi na shauku ya kushuhudia iwapo kuna aliyenusurika katika ajali hiyo, lakini ukweli ulibainika kwamba hakuna abiria aliyekuwa kwenye daladala hiyo aliyekuwa hai.
Mwili wa dereva wa daladala hiyo ulikutwa huku kichwa chake kikiwa kimenasa kwenye vyuma vya matairi ya Veco na ilibidi kukata vyuma vivyo, ili kuutoa lakini miguu yake ikiwa imekatika.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, aliwasili kwenye tukio hilo mapema, na ingawa alionekana akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa na tukio hilo, alimudu kusimamia na kuongoza uondoaji wa miili ya watu kutoka ilipokuwa imekandamizwa na lori hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda Mpinga alisema dereva wa gari lililosababisha ajali hiyo ya kutisha ametoroka, na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili aweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Kwa kweli kama mlivyoona, hadi sasa mimi naweza kusema waliokufa ni watu nane lakini idadi hiyo inaweza kuongezeka kwa sababu mmeona jinsi miili mingine ilivyokatika vipande vipande, hivyo tutaangalia kwa makini zaidi na tutatoa taarifa zaidi,” alisema.
Alisema ajali hiyo imekuwa changamoto kubwa kwake binafsi na kwa Kikosi cha Usalama Barabarani kutokana na kutokuwa na vifaa vya uokoaji vinavyoendana na mazingira ya ajali husika, ikiwa ni pamoja na gari la kuinulia vitu vizito.
“Gari tatu zimekuja hapa lakini zimeshindwa kuinua gari iliyolalia daladala, hii ni hatari kwa sababu hata kama kungekuwa na abiria ambaye amejeruhiwa kidogo na angehitaji kuokolewa na kukimbizwa hospitali kwa matibabu isingewezekana, kwa muda wote huo angekuwa ameshapoteza maisha huku tunamuona,” alisema kwa masikitiko.
Aliongeza kuwa baada ya gari hizo kushindwa kuinua lori hilo, wamelazimika kuomba msaada kutoka BMK Osterbay, na kutokana na uzito wake, ilichukua muda wa saa mbili kufika eneo la ajali, lakini ndilo lililofanikisha kupatikana kwa miili minane ya watu iliyokuwa imelaliwa na lori hilo.
Aliwashukuru polisi kwa kufika haraka kwenye eneo la ajali na kufanikiwa kudhibiti wizi wa mafuta, ambao ulikusudiwa kufanywa na baadhi ya wananchi waliokimbilia katika eneo hilo, hali ambayo ingeweza kusababisha hatari kubwa zaidi.
Miili ya watu hao ilipelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Tumbi wilayani Kibaha na Mwananyamala, wilayani Kinondoni, ambako ndugu na jamaa wanatarajiwa kwenda kuitambua na kufanya taratibu za mazishi.

No comments:
Post a Comment