Habari za Punde

*ALIYENENEPESHA NYETI NA KUFIKIA KG 10, AFANYIWA UPASUAJI INDIA

Na Herrieth Benny

MSHKAJI aliyejaribu kutaka kunenepesha nyeti na kuharibikiwa hadi kufikia zaidi ya kilo10, tofauti na matarajio yake, Gasper Honza, amefanyiwa upasuaji mkubwa juzi nchini India.
Jopo la madaktari zaidi ya 5 wa hospitali hiyo (jina kapuni) wamesema kuwa upasuaji huo wa Gasper, umechukua masaa 14, kutokana na ukubwa wa tatizo lenyewe jambo ambalo limekuwa tofauti zaidi na pasuaji nyingine kutokana na Honza kutokwa na damu nyingi wakati wa upasuaji huo.
Akizungumza na Sufianimafoto Reporter, kwa njia ya simu Dk. Hich Yagien, emesema hali hiyo iliwapa wasi wasi mkubwa, ijapo wamedai kuwa wafanikiwa kumaliza salama.
Kwa mijibu Dk Yagieni, amesema hali hiyo imesababishwa na kemikali iliyokuwamo kwenye dawa aliyotumia kukuzia nyeti hiyo aina ya “hypson”
Hata hivyo anasema wamefanikiwa kumuwekea chembechembe zenye dawa aina ya spinal Growth, zenye uwezo wa kuchochoea na kukuza homoni (mbegu za kiume ) na kusababisha hali ya kuhisi kufanya tendo la ndoa.
“Tusingefanya hivyo Gonza angekuwa hanisi maisha yake yote, pia upasuaji tuliofanya tumeweza kuunganisha nyama za siri, kwa utalamu zaidi hivyo maumbule yake sasa ni kama ya mwanume mwingine yanaujazo kamaili, lakini atahitaji kupumzika kwa muda wa miezi 3 bila kufanya tendo la ndoa” alisema Dokta
Kwa upande wake Gonza alisema anahisi maumivu makali ya kidonda hicho yanayomfanya ashindwe kuzungumza nasi kwa muda “ninamshukuru mungu nimeweza kutoka chumba cha upasuji salama ila nahisi maumivu makali samahani naomba nitafute siku nyingine”alisema Gonza.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.