Habari za Punde

*SIMBA YANG'ARA ZIMBABWE, YAWACHAPA LEIGTHENS 3-0


















Mussa Hassan Mgosi katika moja ya mchezo wa timu yake ya Simba, ambaye ni miongoni mwa wafungaji wa mabao huko Zimbabwe.


Na Sufianimafoto Reporter, Zimbabwe
Simba ya jijini Dar es Salaam, (Wekundu wa Msimbazi) wamefanikiwa kuwachapa wapinzania wao timu ya Leigthens ya Zimbambwe kwa magoli 2-0, katika mchezo wa kombe la Shirikisho uliomalizika hivi punde katika Uwanja wa Rufaro, Harare jijini Zimbabwe.
Magoli 2 ya Simba yamepatikana katika kipindi cha kwanza cha mchezo huku goli la kwanza likiwekwa kimiani na, Mussa Hassan Mgosi na lapili Mohamed Banka, na latatu likiwekwa kimiani na Mohamedi Kijuso katika kipindi cha pili na kuzima kabisa matumaini ya wapinzani wao waliokuwa wakicheza kwa kujiamini zaidi katika dimba la nyumbani. Timu ya Simba iliwakilishwa na wachezaji, Juma Kaseja, Haruna Shamte, Salum Kanoni, Kelvin Yondani, George Owino, Mohamed Banka, Nico Nyagawa, Hiral Echesa, Mussa Hassan Mgosi, Mike Barasa na Ramadhan Chombo.
Nayo timu ya Leigthens iliwakilishwa na:- Lovemore Makuvarara, Tshuma Bruce, Mteki Richard, Mparata Tawanda, Machona Casper, Moyo Godfrey, Nhamo Patrick, Stephano Matsangaise, Dzukamanja Admire, Chivheya Arenold na Nyamiwa Artwell.
Simba inatarajia kuwasili nchini kesho saa tatu asubuhi, baada ya mtanange huo uliomalizika hivi punde.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.