Habari za Punde

*TWIGA STARS WAFUZU BAADA YA KUWATOA ETHIOPIA

*Waethiopia wageuka mabondia uwanjani.......Asha, apiga goli la kioo











Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, wakishangilia kwa staili ya kusali katikati ya uwanja mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati yao na Ethiopia, baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na kuwafanya kusonga mbele katika Michuano ya awali ya Kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia kwa wanawake 2010, ambapo sasa Twiga Stars anatarajia kukutana na Elitria. Katika mchezo wa awali baina ya Twiga na Ethiopia uliochezwa Ethiopia, Twiga ilishinda mabao, 3-1.

"Kushinda raha jamaniiii eeeeh!"











Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, George Mkuchika na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margareth Sitta (katikati) wakipiga picha ya kumbukumbu kwa furaha na wachezaji wa Twiga, mara baada ya mchezo huo kumalizika.












Mchezaji wa Ethiopia, akilia kwa uchungu mara baada ya timu yake kufungwa bao la kusawazisha kwa njia ya adhabu katika kipindi cha pili.









Kocha wa Ethiopia na wachezaji wake wakiwa hawaamini kilichotokea na kinachoendelea uwanjani baada ya wachezaji wake kuanza vurugu wakikataa goli, jambo ambalo liliwafanya baadhi ya viongozi wa timu hiyo kuingia katikati ya uwanja na askari kuingia kati ili kuwaondoa waethiopia hao.










Askari Polisi wakiwaondoa wachezaji wa akiba wa Ethiopia na viongozi wao walioingia katikati ya uwanja kumzonga refa wakati wa mchezo ukiendelea, wakigomea goli lililofungwa na Asha kwa njia wa adhabu.












Haya ni mapozi ya kupiga picha, Emmanuel Ndege wa gazeti la Uhuru, akipiga picha kwa staili ya kukwepa ngumi ya mmoja wa viongozi wa Ethiopia (katikati) aliyetaka kumtwanga ngumi akimzuia kupiga picha wakati waethiopia hao walipokuwa wakifanya vurugu uwanjani hapo.












Wachezaji wa akiba wa Ethiopia wakiwatishia wapiga picha kuwapiga na chupa za maji huku wakitukana matusi kwa lugha yao, ambayo hayakuweza kumsumbua mtu kwani wapiga picha walio kuwapo uwanjani hapo wengi wao hawakuielewa lugha iliyokuwa ikitumika kuwatukana.











Hili ndilo goli lililozua utata, lililopigwa na Asha Abdallah kwa njia ya adhabu ndogo, huyu ni kipa wa Ethiopia akishangaa bila jitihada za kujaribu kuuokoa mpira huo uliopiga besela ya juu kwa ndani na kisha kudondoka kwenye nyavu ndogo nyuma ya mstari wa milingoti ya goli.

"Kudadadek! nimeukosa"









Kiungo mshambuliaji wa Twiga Stars, Ester Chabruma (kulia) akijitahidi kujikunja kuupiga mpira kwa kichwa baada ya krosi nzuri iliyopigwa na beki wa kulia wa Twiga, na kudondoka ndani ya 18, hata hivyo Ester aliukosa mpira huo na hivyo kukosa goli la wazi, na kuwafanya mashabiki waliokuwapo uwanjani hapo kuzua makelele na minongono.













Beki wa Ethiopia, (kushoto) akijaribu kumdhibiti mshambuliaji wa Twiga Stars, Asha Abdallah, wakati wa mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.