Huyu si mwingine ni mpiga picha wa gazeti la Habari Leo, Mroki Mroki almaaruf Mr. Kidevu, akihangaika na kamera iliyoonekana kumzidia nguvu na kuamua kuifunga mpira katika chuma huku akijihisi ameweka kamera hiyo katika stendi, "ahaa hapa sasa napata picha vizuri" alisikika akisema Mroki. Na nyie waajiri tunashukuru iwapo mnatambua umuhimu wa wapiga picha katika vyombo vya habari, basi jitahidini kuboresha vitendea kazi na iwapo mmefanikiwa kununua kifaa kama hiki, iweje mshindwe kununua na stendi yake hali yakuwa mnafahamu umuhimu wake?, Je akileta picha zote zimeshake mtamlaumu? TUHESHIMIANE KATIKA KAZI kila mmoja katika nafasi yake.
Meya ‘Shetta’ kuja na goli la Meya
-
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam Nurdin Bilal ‘Shetta’, amesema milango ya
ofisi yake iko wazi kwa wasanii na wanamichezo kwa jambo lolote
linaliweza ku...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment