Paul Kimiti (Mb) ambaye pia ni rafiki na mshauri wa familia ya kampuni ya Mabibo, akicheza dansi na mwimbaji wa Fm Academia, Nyosh El-Saadat, wakati wa hafla maalum ya shukrani kwa wadau na wanahabari iliyoandaliwa na kampuni ya Mabibo Beer Wines & Spirits Ltd, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi za Heineken Mikocheni Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines & Spirits Ltd - Benedicta Rugemalira, akisoma hoyuba yake kwa wageni waalikwa na wafanyakazi wa Kampuni hiyo wakati wa hafla hiyo.
Wasanii wa kundi la Promosheni la Kampuni hiyo ya Heineken, wakishambulia jukwaa wakati wa hafla hiyo.
Mc Thabit Ally, akionyesha umahiri wake wa kucheza na kuimba Hip Hop, muziki wa John Walker, "Hii Kitu Hii Kitu Hii"....
Wanenguaji wa Fm Academia, wakishambulia jukwaa wakati wa hafla hiyo.
Wanenguaji wa Fm, kutoka kushoto, Charleme Yenge, Aaliyah na Stefam Nguya, wakipozi kwa picha kabla ya onyesha hilo kuanza kushambulia jukwaa.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia hafla hiyo, wakipombeka kama unavyoona meza yao ikiwa imesheheni vilaji.
Rais wa Fm Academia, Nyoshi El Saadat, akiwachezesha wakurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer.
Hii ni Hip Hop Dance kutoka kwa kundi la Promosheni la Heineken.
Hii ni miondoko ya South ya kundi hilo.
Na Sufianimafoto, Jijini Dar es Salaam
KAMPUNI ya Mabibo Beer Wines & Spirits Ltd imeweka mikakati maalumu katika kuhakikisha inalinda soko la vinywaji vyake hatua ambayo pamoja na mambo mengine itasaidia kulinda ubora wake kwa pamoja na afya ya wanywaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Benedicta Rugemalira alisema tayari wameweka mipango maalumu kuhakikisha wanafanikiwa katika hilo ambapo aliomba ushirikiano kutoka kwa wadau wa biashara na wananchi kwa ujumla.
Mkurugenzi huyo aliyasema hayo katika hafla ya shukrani kwa wadau mbalimbali wa sekta ya biashara na habari iliyoandaliwa na kampuni hiyo mwishoni mwa wiki Dar es Salaam.
Alisema biashara ya vinywaji imekuwa ikikua kwa kasi nchini hivyo kuongeza ushindani na kwamba MABIBO imejidhatiti kuhakikisha haki ya pekee iliyonayo ya kuingiza nchini bia za Heineken na Windhoek haingiliwi ambapo alitoa angalizo kwa wafanyabiashara kutoingia katika mtego huo kwani mkono wa sheria utawawajibisha.
“Tumekuwa na mipango ya kujilinda kisoko kwa muda wote lakini kwa kadri siku zinavyokwenda ushindani wa kibiashara unaendelea kukua hivyo nasi tumeona tuongeze nguvu katika hili na kwakuwa hii ni sawa na vita basi mbinu hizi ni siri yetu lakini kwenu nyinyi kama wadau tunaomba tushirikiane,” alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake mgeni rasmi Paul Kimiti ambaye ni rafiki na mshauri wa kampuni hiyo kwa siku nyingi aliwataka watanzania kuwaunga mkono watanzania wanaojitokeza kuwekeza katika biashara kama ilivyo MABIBO na kushauri kutumia vinywaji venye viwango vya ubora wa kimatiafa kwani ndivyo sahihi kwa afya zao.
Aliitaka kampuni hiyo iendelee kubuni njia mbalimbali za kuhakikisha biashara hiyo inaendelea kukua na kwamba wasikatishwe tamaa na wafanyabiashara wachache wanaokiuka taratibu na sheria za sekta hiyo.
“Tutafanya jambo la faraja na kujivunia iwapo watanzania sote kwa ujumla wetu tutajijengea tabia ya kuwaunga mkono wenzetu wachache wanaowekeza katika biashara kwani pamoja na faida binafsi wanayopata pia nchi inafaidika,” alisema Kimiti.
Akifafanua kuhusu mikakati yao wakili wa kampuni hiyo Respicius Didace alisema ni pamoja na kuweka makubaliano maalumu na Jeshi la Polisi kwa pamoja na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ili kudhibiti wahujumu wanotumia ‘njia za panya’ kuingiza vinywaji hivyo nchini .
“Tayari tumefanya makubaliano na vyombo vinavyohusika na hivi sasa bia ya Heineken ya shingo fupi ni maalumu kwajili ya taasisi na mashirika maalumu hivyo hairuhusiwi kuuzwa katika soko la kawaida,” alisema.
Aliongeza kuwa wafanyabiashara wapo huru kununua na kuuza bia za Heineken za shingo ndefu pamoja na zile za Windhoek ambapo aliwaomba wadau wao kuwa askari kanzu wa kutoa taarifa za wale wanaoihujumu kampuni hiyo.

No comments:
Post a Comment