Ofisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air, Alphose Kioko (kushototo) alikamkabidhi zawadi, mwakilishi wa wakala wa usafirishaji wa kampuni ya Bon Voyage, Nafisa Mohamed, kwa kuibuka mshindi kati ya Mawakala wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na Kampuni ya Precision Air mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kutambua mchango wa mawakala hao.
Wafanyakazi hao wakiselebuka wakati wa hafla hiyo, hapa ni sebene kwa kwenda mbeleeeeee.
Hawa ni baadhi ya wafanyakazi hao wakisubiri kupewa tuzo.
Tuzo kwa waliofanya vizuri.
*KAMPUNI YA NDEGE YA PRECISION AIR KUANZA SAFARI ZA SOUTH NA HARARE
Precision Air shirika la ndege linaloongoza Tanzania lina mpango wa kununua ndege nyingine aina ya Boing 737 baadaye mwaka huu na kuanzisha safari za Johannesburg, Afrika Kusini na Lusaka, Harare.
Precision Air pia ina mpango wa kununua ndege nyingine mpya tano aina ya ATR katika kipindi cha miaka miwili ijayo, ikiwa ni sehemu ya mpango wake kabambe wa kuongeza idadi ya ndege zake.
Mipango hiyo ya kukua kwa biashara ya Precision Air ilitangazwa mwisho mwa wiki na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Alphonse Kioko wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa maalum kwa ajili ya Mawakala wa Precision Air wa Usafirishaji ili kuwapongeza kwa ajili ya mchango wao kwa biashara ya shirika hilo la ndege.
‘’Tulianza na mpango wa kuboresha ndege zetu mwaka 2006 tulipoingia mkataba wa Dola za Marekani 129 milioni na ATR ya Ufaransa ili ituletee ndege mpya saba. Kati ya hizo ndege saba tayari tunazo tano, na mbili za mwisho zitaletwa mwezi juni na julai mwaka huu. Usafiri wetu utaweza kutegemewa zaidi,na tutazingatia zaidi muda , kadhalika wasafiri wataburudika sana kwa sababu ndege zetu mpya zina burudani ndani kwa safari fupi,’’ alisema Kioko.
‘’Precision Air imekuwa ikipata faida ya zaidi ya asilimia kumi kila mwaka kwa sababu ya mchango wa mawakala wetu wa usafirishaji,’’ Kioka alisema na kuongeza ‘’ Watu wanaothubutu kuota ndio watakaohimili ushindani na biashara itatawaliwa na wale wanaothubutu kuota na kutekeleza ndoto zao, ni matumaini yangu tutaendelea kuota pamoja kwa sababu utekelezaji wa ndoto hizo unatoa gawio,’’ alisema Kioko na kuongeza kwamba wana mpango wa kuanzisha huduma ya SMS ili wateja wapate taarifa mbali mbali kuhusu safari za ndege kwa urahisi zaidi kupitia simu za mkononi.
Katika hafla hiyo kampauni ya Uwakala wa Usafirishaji ya Bon Voyage Travels ndio waliotangaza washindi wakiongoza kwa mauzo ya tike za Precission Air na wapipewa Tuzo pamoja na mawakala wengine wote za kutambua mchango wao kwa biashata ya Preccision Air.
Shirika la ndege la Precision lina mtandao unaoongoza wa safari za ndani ya nchi ukiwa na safari za Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibar, Mwanza, Kigoma, Tabora, Musoma, Shinyanga, Mtwara. Precision Air pia ina safari za Nairobi, Mombasa na Entebbe

No comments:
Post a Comment