Kipa wa Somalia, Kamal Ali Omer, akijitahidi kuokoa mpira uliopigwa na Mussa Hassan Mgosi, uliokuwa ukitinga wavuni bila mafanikio, wakati wa mchezo wa kufuzu kucheza michuano ya CHAN, itakayofanyia nchini Sudan mwakani, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam leo jioni. Stars imeshinda 6-0.
Mshambuliaji wa Stars, John Boko, akimtoka beki wa Somali, Mohamed Moshi Siyod, wakati wa mchezo huo.
Mrisho Ngassa, akimtesa kipa wa Somari kwa kufunga goli la tatu kati ya sita yaliyofungwa na Taifa Stars.
John Boko (kulia) na Mrisho Ngassa, wakishangia goli lililofungwa na Ngassa.
Arasto Nyoni, akishangilia goli lake alilofunga katika kipindi cha pili cha mchezo.
Mshambuliaji wa Taifa Stars, Mussa Hassan Mgosi, akimtoka beki wa Somalia, Hussein Ali Roble, wakati wa mchezo huo.
"Du hii mijamaa ni noma inakaza namna hii, mbona Nairobi haikuwa hivi? aah mwache apite tu mie hoi hapa"
No comments:
Post a Comment