Sehemu ya Bango la Tangazo la huduma hiyo linavyoonekana.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mahusiano na Vodacom Faundation, Mwamvita Makamba (kulia) akizungumza wakati wa ziara yao ya kutangaza uzinduzi wa huduma hiyo mpya. Katikati ni Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Simu za mkononi, Vodacom, Ephraim Mafuru, (kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Shailen Salgaonkar.
"EbwanaeeeeH, tumeipenda hiyo itatusaidia sana sisi watumiaji wa VODACOM".
Mhariri Mtendaji wa kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Mhingo Rweyemamu (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha pamoja na wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Vodacom, wakati walipokuwa wakitangaza kuzindua huduma mpya ya kupiga simu kwa gharama nafuu kwa watumiaji wa simu za mtandao huo Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Shailen Salgaonkar (kushoto), Mkurgenzi Masoko wa Kampuni ya Vodacom, Ephraim Mafuru (katikati) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mahusiano na Vodacom Faundation, Mwamvita Makamba, wakionyesha Bango la tangazo la huduma mpya ya kupiga simu kwa gharama nafuu kwa watumiaji wa simu za mtandao huo, wakati wakitangaza kuzindua huduma hiyo.
"Haina shaka kutumia hili neno, huyu jamaa anamkataba wa mwaka mzima na VODACOM, na amefurahi sana kwa kweli Habari ndo hii sasa"
Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom, Ephraim Mafuru (katikati), akifafanua kuhusua matumizi ya msemo wa msanii wa muziki wa kizazi kipya AY, Habari ndo hii, ambaye ameingia mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni hiyo kwa ajili ya kutangaza huduma hiyo katika redio mabango na Televisheni.
No comments:
Post a Comment