Habari za Punde

*ASKARI WALIOWAUA MAJAMBAZI TARIME WATUNUKIWA



Na Christopher Gamaina, Tarime

JESHI la Polisi limewatunukia vyeti na fedha taslimu askari 11 wa jeshi hilo walionyesha ujasiri wa kupambana na hatimaye kuyaua majambazi katika Mkoa wa Kipolisi Tarime,Rorya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hafla hiyo ya kuwapongeza na kuwakabidhi tuzo hizo ilifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya CMG, mjini Tarime, huku kila askari aliyeshiriki zoezi hilo alizawadiwa cheti cha ujasiri na fedha taslimu Sh 100,000.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Constantine Massawe, alisema jeshi hilo limetoa tuzo hizo baada ya askari hao kuonyesha ujasiri mkubwa wa kukabiliana na majambazi katika kitongoji cha Ntagacha wilayani Tarime.
Katika tukio hilo lililotokea Aprili 2, mwaka huu, askari hao walipambano ya kufyatuliana risasi na majambazi hao na kufanikiwa kuyaua na kujeruhi baadhi ya majambazi na hatimaye kufanikiwa kuokoa ng’ombe 11 waliokuwa wameporwa na majambazi hao.
"Utamaduni wa Jeshi la Polisi ni kwamba, huwa anaadabishwa kwa kupewa adhabu pale anapoonekana kutenda kosa na pia ni wajibu wa uongozi kumtunuku askari huyu huyu pindi anapoonekana kufanya vizuri kiutendaji 'kumpongeza'hivyo hawa tuliowapongeza wamefanya kitendo cha ujasiri mkubwa,” alisema Kamanda Massawe"
Aidha, Kamanda Massawe alisema jeshi hilo pia limeshawapongeza kwa kuwapatia zawadi ya fedha taslimu raia wema waliotoa taarifa zilizosaidia kufuatilia tukio hilo la ujambazi.
Kwa upande wake, mgeni rasmi katika hafla hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime, Ernest Kabohola, aliwapongeza askari hao akisema kitendo walichofanya ni cha ujasiri, uadilifu, uzalendo na moyo wa kujituma.
Aliwataka askari wengine kuiga mfano huona kusisitiza kuwa mapambano hayo yawe endelevu ili kukomesha matukio ya ujambazi yakiwamo mauaji ya watu na wizi wa mifugo katika yaliyokithili katika mkoa huo wa Kipolisi.
Viongozi wengine walioshiriki katika hafla hiyo iliyowashirikisha askari 70 ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Paul Ntobi, SSP Benedict Kitalika, Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), ASP Benedict Sungu, Mkuu wa Kikosi cha kudhibiti WIZI WA Mifugo, ASP Simon Mrashani na Mkuu wa Gereza la Tarime, SP Boyd Mwambingu

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.