Na Sufianimafoto Reporter, Ukraine
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Mbaruku Kheri, mwishoni mwa wiki alidundwa na bondia Vital Rusal wa Ukraine, katika pambano lisilokuwa la ubingwa la raundi nane kwa KO.
Kheri alipigwa katika sekunde ya 30 raundi ya kwanza katika pambano lililofanyika ukumbi wa Sport Palace, uliopo nchini Ukraine.
Akizungumza kwa simu kutoka Ukraine, wakala wa Kheri, Franklyn Imbenzi, alisema kuwa bondia huyo alipoteza pambano hilo kutokana na kuzidiwa uwezo na Rusal.
“Hatuwezi kumlaumu Kheri kwa kuvunja rekodi kupoteza mchezo katika sekunde ya 30 ya mchezo raundi ya kwanza, unajua katika mchezo kuna kushindwa, kushinda na sare, yote yanaweza kutokea,” alisema.
Kheri alipigwa katika raundi ya kwanza ya mchezo huo, baada ya kupigwa ngumi tano mfululizo bila majibu ndani ya sekunde hizo 30.
“Rusal hakupata kazi kubwa kumpiga Kheri, ilikuwa katika sekunde ya 30 tu kwani alipigwa ngumi mfululizo na kuanguka chini,” alisema Imbenzi.
Rusal amepigana mapambano 26, kati ya hayo, 10 ameshindwa kwa KO.
Tutaunda timu maalumu kufuatilia hali ya upatikanaji wa Maji mji Soni
wilayani Lushoto-Waziri Aweso
-
Na Oscar Assenga,Lushoto
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema ataunda timu maalumu ili kufuatilia hali
ya upatikanaji wa huduma ya maji katika eneo la Soni...
26 minutes ago
No comments:
Post a Comment