Askari wa zima moto wa Kampuni ya Altmate Security, wakifika eneo la tukio baada ya saa moja tangu kutokea kwa moto huo uliosababishwa na mafundi waliokuwa wakichomelea ndani ya jengo hilo na hatimaye cheche kuruka na kutua katika maboksi yaliyokuwapo eneo hilo na kuzua kizaa zaa cha takriban masaa 4 huku wafanyakazi wa benki hiyo wakiwa nje ya jengo hilo wasijue la kufanya na baadhi ya kinamama wakisikika kulalama kuwa wamesahau 'Hand bag' zao ndani ya ofisi hizo.
Wafanyakazi wa benki hiyo wakiwa nje ya jengo la benki hiyo wakisubiri muafaka kabla ya kurejea kuendelea na kazi.
Baadhi ya wafanyakazi hao wakiangalia moshi uliokuwa ukitoka katika madirisha ya jengo hilo, huku ukiongezeka kwa kasi hali ya kuwa ilielezwa kuwa tayari uliokuwa meshazimwa moto huo kabla hata ya kufika kwa wazima moto.
No comments:
Post a Comment