Habari za Punde

*tiGO YAZINDUA PROMOSHENI YA SAJILI NA USHINDE


Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi Tigo, Jackson Mbando, (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati wa kutangaza Kampeni ya Promosheni ya ‘Sajili na Ushinde’ inayoanza Mei 25 mwaka huu, ambapo mteja wa mtandao huo anaweza kujishindia zawadi za pikipiki, muda wa maongezi na Nyumba. Kulia ni Meneja wa huduma kwa wateja wa Tigo, Harriet Lwakatare.

Jackson (kushoto) na Harriet, wakitoa maelekezo ya jinsi ya kutuma ujumbe ili kuingia katika Droo ya Promosheni hiyo.
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imezindua promosheni maalum ka wateja wake wote wanaosali namba zao za simu ikiwa na lengo la kuhimiza zoezi hilo kwa wateja wote nchini
akiongea na waandishi wa habari Afisa uhusiano wa Tigo Tanzania Jackson Mmbando alisema ‘’Tigo tumeamua kuanzisha promosheni hii maalum kwa wateja wetu ili kuwahimiza wateja wote nchini kufanya usajili wa namba zao mapema kama vile ilivyoagizwa na serikali.
tunaamini kwamba kupitia promosheni hii tutazawadia wateja wetu wote waliodumu na familia ya Tigo kwa kipindi kirefu
Promosheni hii itaanza rasmi leo Aprili 23 hadi 30 juni 2010 ambapo tunatarajia kila mteja wetu atakuwa amesajili namba yake.tutatoa muda wa maongeze vifurushi 3,600,000 hii itakuwa ni idadi ya wateja watakaopata vifurushi hivyo vya dakika 3, 15, 80, 150 or 300 za muda wa maongezi tigo-tigo
pia kutakuwa na zawadi kubwa zitakazotolewa kwenye droo tofauti zitakazofanyika kwa mfuatano ambapo wateja wote WALIOSAJILI watashindania pikipiki 10, gari mpya Grand Vitara 3 au Nyumba nzuri yenye gharama ya hadi milioni mia moja
kushiriki promosheni hii ya Sajili na Ushinde ni rahisi na pia ni bure, unachotakiwa kufanya ni kwenda kusali namba yako kwa wakala wetu, ofisi za huduma za wateja au maduka maalum ya usajili yaliyoko sehemu mbalimbali.
Kisha utatakiwa kutuma namba yako ya fomu ya USALI kwenda 15150 bure ili uweze kuingia kwenye droo zetu za SAJILI na Ushinde
kama tayari ulishasajili namba yako tangu zamani unatakiwa kutuma namba yako ya fomu kwenda namba 15150 na utaingizwa kwenye droo zetu pia
Droo zetu ni kama ifuatavyo
Droo ya kwanza: 25 Mei 2010 –pikipiki tatu pamoja na gari moja (Grand Vitara mpya)
Yapili: 29 June 2010 - pikipiki tatu pamoja na gari moja (Grand Vitara mpya)
YaTatu: 28 Julai 2010 - pikipiki nne pamoja na gari moja (Grand Vitara mpya)
Droo Kubwa : 4 August 2010 – nyumba moja yenye thamani ya hadi milioni 100 kwenye sehemu au mji atakapopatikana mshindi wetu.
Hii ni kwa Tigo tu kwamba kwakujisali namba yako Tigo inaboresha maisha yako ,
Anza kutuma namba yako ya uajili kuanzia sasa hadi 30 juni 2010 muda wowote
Zawadi zetu zitakuwa zikikabidhiwa hapa Dar es salaam lakini ile ya nyumba itakabidhiwa mahali anakopatikana mshindi .
Vigezo vingine vya promosheni hii maalumu kwa wateja wa tigo ni kwamba wafanyakazi a tigo pamoja na familia zao hawarudusiwi kushiriki, majina ya washindi yatatangazwa kwenye biombo vya habari kila baada ya droo. Mshindi wa pikipiki, gari au nyumba atatakiwa kuonyesha uthibitisho wa nakala ya usajili pamoja na kitambulisho chake halisi kama ilivyo kwenye fomu ya usajili ili kukabidhiwa zawadi yake.
Unatakiwa kujiunga na promosheni hii mara moja tu kwa kila laini yako iliyosajiliwa, pia kumbuka kwamba kila mteja anaweza kushinda muda wa maongezi wa dakika 3, 15, 80, 150 or 300 papo hapo akituma namba yake ya usajili kwenda 15150 na pia ataendelea kuwa na nafasi ya kujishindia pikipiki, gari, au Nyumba.
Mshiriki yeyote atashinda zawadi kubwa mara moja yaani pikipiki au gari au nyumba na hatoweza kushinda mara mbili
Nyumba yenye thamani ya hadi milioni 100 itanunuliwa kwenye eneo analopatikana mshindi wetu wa SAJILI na USHINDE na ieleweke kuwa zawadi zote haziwezi kukabidhiwa kwenye mfumo wa pesa.
Kila mwenye laini ya Tigo anaweza kushiriki promosheni ya TIGO SAJILI na USHINDE lakini watoto wenye miaka chini ya 18 hawaruhusiwi kwa mujibu wa bodi ya michezo ya kubahatisha.
Mwisho wa kujichukulia zawadi katika promosheni hii ni septemba 2010



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.