Habari za Punde

*MATUKIO YA JIJINI DAR ES SALAAM LEO KATIKA PICHA

*HAWA MGAMBO SASA NI NOMA, BIASHARA ZA WAMACHINGA WAO WAMEFANYA MTAJI.

Mgambo wa Manispaa ya Ilala, wakiwanyang’anya makoti wafanyabiashara kwenye mtaa wa Samora Dar es Salaam leo. Mgambo hao walikuwa wakiwanyatia wafanyabiashara hao mithili ya Chui ama samba anavyomnyatia Swala na kufanikiwa kumdaka jamaa mmoja aliyekuwa amejisahau na kumkwapua makoti na kuondoka nayo, Je makoti hayo na biashara nyingine walizokwisha wapora machinga zinafika sehemu husika kweli?

Mgambo wa kike akiondoka na makoti hayo baada ya kukabidhiwa na mgambo wa kiume aliyefanya kazi ya kuwapora wafanyabiashara hao.
*MIUNDOMBINU YA MWAKA 47 YAWA KERO JIJINI DAR ES SALAAM.
Pamoja na jitihada za Manispaa za jiji kujitahidi kujenga mitaro katika baadhi ya maeneo ya jiji, lakiini bado eneo hili la katikati ya Jiji Posta, huwa limekuwa likishindikana na hasa kwa kipindi hiki cha mvua ambapo eneo hili hujaa maji hadi kuharibu barabara hiyo ya mbele ya Jengo la Hidary Plaza. Pichani ni mafundi wakijitahidi kuzamisha mikono yao kwenye maji hayo yaliyotuama ili kuzibua mtaro wa kupitishia maji yaweze kupungua eneo hilo.

“MSIREKEBISHE ILIMRADI TU SIKU IENDE MUINGIZE PESA, REKEBISHENI NA ZIWAKE”

Mafundi wakirekebisha taa ya barabarani iliyopo mbele ya Hospitali ya Agakhan Dar es Salaam leo mchana. Mataa mengi yaliyopo kwenye barabara za jijini zimekuwa kama mapambo kwani nyingi huwa haziwaki ifikapo jioni na hata zile mpya zilizowekwa barabara ya Sam Nujoma zikionekana za kisasa zaidi na hasa kwa kutumia mionzi ya jua Sola Pawa nazo kwa sasa zimekuwa zikiwaka kwa mafungu huku semu nyingine ya barabara hiyo ikibaki na kiza Totoro.
*WAZUNGU NAO WAKATI MWINGINE HUWA WANACHEMKA, MZUNGU ABANA NYWELE KWA KUTUMIA PENI.
Hii ilikuwa ni kwenye daladala linalofanya safari zake Mwenge Posta kupitia Sinza, wakati Sufianimafoto alipopanda daladala hilo na kukutana mchemko huo, Mzungu huyu akiwa katulia tuuuli katika siti ya mbele huku akipiga story na Mmasai, akiwa amebana nywele zake kwa kutumia peni tena nyekundu ambayo huonekana na kila mmoja atakayebahatika kutupia macho katika kichwa hicho, Je angekuwa ni mswahili amefanya hivyo si ingekuwa gumzo gari zima? kama unavyojua hata katika hali ya kawaida mbongo anapovaa kandambili na kuingia katika Hoteli yeyote kubwa huzuiliwa, lakini anapovaa mzungu atapita tu tena bila hata kuulizwa chochote, sasa sijui huwa hata walinzi huogopa lugha ama ni utamaduni gani?.
*MAAJABU YA DUNIANI
Gari ikiwa imechoma kwenye ukuta wa nyumba ya ghorofa huko Duniani, haikuweza kufahamika gari hiii ilikuwa ikipaa ama ilipita wapi hadi kugonga ukuta huu tena juu.







No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.