Habari za Punde

*WAZIRI MKUU ZIARANI SINGIDA, MASISTA WAMUANDALIA IBADA MAALUM

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe, Tunu Pinda, wakiwa katika Ibada fupi iliyoandaliwa na Masister wa Shirika la Ursula la Mkiwa, Singida baada ya kupokea taarifa ya wilaya hiyo kwenye ukumbi wa Masista hao juzi, wakati wakiwa kwenye ziara ya mkoa huo. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kushoto) wakikagua shamba darasa la Alizeti la Mzee Napegwe Shilla wa kijiji cha Nkalakala wilayani Iramba, akiwa katika ziara ya mkoa wa Singida juzi.

Waziri Mkuu na Mkewe Tunu (kushoto kwake) wakisikiliza wimbo kutoka kwa wanakwaya waliokuwa wamebeba shina la muhogo baada ya kuwasili kwenye shule ya Sekondari ya Iguguno wilayani Iramba wakiwa katika ziara ya Mkoa wa Singida Mwenye miwani kushoto ni mkuu wa Mkoa huo, Parseko Ole Kone.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.