Habari za Punde

*SAFARI YA KUELEKEA NYUMBANI KWA VODA MILIONEA 2010, MOROGORO

Mshindi wa Tuzo Milionea 2010, Benard John(27) mkazi wa Morogoro, (katika) akizungumza na Mtaalamu wa mambo ya habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (kushoto)na Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nector Foya wakati walipomtembelea nyumbani kwake Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya kumkabidhi kitita chake cha Milioni 100 alizoshinda katika Droo ya ‘TUZO MILIONEA’ iliyomalizika hivi karibuni.

Wakianza kuona mandhali ya mji wa Morogoro.

Tayari msafara mzima wa Wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi VODACOM, umekwishaingia mjini Morogoro, tayari kufika nyumbani kwa Voda Milionea kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kumkabidhi kitita chake alichoshinda katika Droo hiyo iliyomalizika hivi karibuni.

Gari lililokuwa na wafanyakazi wa Vodacom, likiingia nyumbani kwa Voda Milionea, Bw. Benald John.

Bwana John (katikati) akiwakaribisha watu wa Vodacom kwa furaha nyumbani kwake, huku akiwaongoza kuingia ndani tayari kwa mazungumzo.

Baada ya kufiaka uwani alisalimiana na kumkaribisha, Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nector Foya.

Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nector Foya (kushoto) akisalimiana na ndugu na jamaa wa John nyumbani hapo.

Msafara huo ukizungushwa katika kona za nyumba hiyo kukagua na kujionea mazingira ya nyumba ya bw. Voda Milionea.

Haya ndiyo mazingira halisi ya nyumba hiyo kwa nje.

Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nector Foya (kushoto) akizungumza jambo kumueleza bw. John kile kilichowafanya kusafiri kutoka Dar mpaka Moro.

"Hapa ndo chumbani kwangu jamani"

Bw, John akifurahi na kufafanua machache akiwa katika chumba chake halisi anachopatia usingizi wa kila siku.

Na hapa ndiyo sebuleni kwa Bw, John kama unavyoona TV, Jiko na baadhi ya vitu.

"Ahsante saaaana, kwaheri na karibu tena hapa nyumbani orogoro"
Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nector Foya, akiagana na Bw. John baada ya kumaliza taratibu zote na kueleza lengo la safari yao.

Baadhi ya nyumba za mji wa Morogoro na milima.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.