Haya yalikuwa ni mapozi ya kuangalia mandhali nzuri ya Hoteli ya South Beach Resort, baada ya kuwasili kwenye ufukwe huo kwa ajili ya kushiriki Semina iliyoandaliwa maalum na Kampuni ya Bia ya TBL, kwa ajili ya kujadili, kuhisiana na kujifunza ili kuboresha michuano ya Kili Taifa Cup inayotarajia kuanza Mei 8 hadi 31 mwaka huu, Ebwanaeeh! huyu si mwingine ndiye Sufianimafoto akiwa katika pozi takatifu.
"Nadhani mtakuwa mmenielewa au siyo jamani?"
Mkurugenzi Masoko wa TBL. David Minja, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Semina hiyo kwa ajili ya michuano ya Kili Taifa Cup iliyofanyika kenye Hoteli ya South Beach Resort Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. Kampuni hiyo kwa mwaka huu imeandaa jumla ya Shilingi milioni 850 ikiwa ni sehemu ya kuboresha michuano hiyo iliyoanzishwa mwaka 1950, wakati huo ikiitwa SUNLIGHT CUP.
Safari ya kuelekea katika Semina hiyo ilianza hivi
Safari ya kuelekea katika Semina hiyo ilianza hivi
Hawa ni baadhi ya waandishi wa habari wakiwa wamejichanganya na wakazi wa Kigamboni, wakati wakitelemka kwenye Kivuko cha Mv Magogoni, kuelekea South Beach.
"Kabla ya kusherehekea kwanza tupambe"
Hawa ni baadhi tu ya waandishi wakijiburudisha na kifungua kinywa baada ya kuwasili South Beach, kabla ya kuanza libeneke la Semina hiyo.
Wakati wengine wakiendelea na zoezi la kupata Break Fast, wengine bado walikuwa katika zoezi la kuhakiki vitambulisho vyao, hii ni kuonyesha ni jinsi gani Kampuni ya Executive Solution, ilikuwa imejiandaa vya kutosha kuhakikisha hakuna Kanjanja atakayezamia katika shughuli hiyo na kupunguza kile kilichoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa ukweli.
"Sasa tunaanza jamani eeeh!"
Huyu alikuwa ni msema chochote wa shughuli hiyo ama Mshereheshaji akiendesha ratiba ya semina hiyo.
Kuonyesha ni jinsi gani Kilimanjaro kwa kushirikiana na Kampuni ya Executive Solution, wanatambua umuhimu wa habari na vyombo vyote vinavyohusiana na habari, pia waliweza kutoa mialiko kwa wamiliki wa Blogs, huyu si mwingine ni Mzee wa mtaa kwa mtaa blogspot, akipandisha kila kinachojiri katika semina hiyo wakati ikiendelea ukumbini hapo.
Hawa ni baadhi ya waandishi wa habari na wapigapicha wakifuatilia kwa makini kila kinachoelezwa ukumbini humo.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa Semina hiyo.
Semina hiyo pia walialikwa watu wa shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kutoa mawili matatu ikiwa ni pamoja na kanuni za mashindano hayo, huyu si mwingine ni Katibu Mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela, akifafanua jambo.
Mwandishi wa Star Tv, Neema (kushoto) Moland na Tulo Chananiliu, wakiwa ukumbini humo.
Baada ya mazungumzo marefu ulifika muda wa msosi ambapo kila mmoja alikuwa bize kujisevia maakuli ili kujiweka sawa kwa ajili ya kurejea katika ngwe ya pili ya Semina hiyo.
Wakiendelea kujisevia.
"Hapa ni msosi tu haina kulemba babake"
Ebwana eeh mshikaji kwa upande wangu mie sikuweza kuamini macho yangu kwa kile nilichokuwa nikiona mbele ya macho yangu, jinsi mshkaji huyu alivyojisevia hadi kupitiliza, kwani nilihisi alibeba kwa ajili ya kula na mwenzie aliyeona uvivu kujongea kwenye meza ya Bufee, kumbe mchizi duh!...., eti hii ndo Kambi ya Ngumi ya Ilala, Ashanti "Unazani kuanzisha Kambi ya Ngumi mchezo siyo mambo yenyewe ndo kama haya, ukikipata kitumie na ukikikosa kijutie" alisema jamaa huyo baada ya kuona kila mmoja akimtolea mimacho na kuhoji oyaaa mpo wangapi msosi huo??????
Awamu ya pili.......
Meneja wa Kampuni inayodili na waandishi wa habari katika Michuano hiyo, Thomson, naye pia hakuwa nyuma katika kueleza machache anayoyafahamu juu ya kuripoti Kili Taifa Cup.
Washkaji wakisikiliza kwa mbwembwe, lakini sasa sijui shibe mwana malevya?????
Ebwana eeh! picha za kumbukumbi pia ilikuwa ni muhimu (wapili kushoto) ni Sufianimafoto, akipiga picha ya kumbukumbi na baadhi ya waandishi na wapigapicha wa vyombo mbalimbali waliohudhuliwa Semina hiyo, So inaonekana Kili Taifa Cup ya mwaka huu itakuwa bomba kupitiliza lakini iwapo waandaaji watawawezesha waandishi hawa waliowanoa katika semina hii, MTUWEZESHE NASI TUWAWEZESHE au siyo?????
Baada ya yooote ilikuwa ni burudani ya Soka, Yanga na Simba
Baada ya makubaliano kipute kiliwekwa ufukweni na kupigwa kwa upinzani mkubwa baina ya mashabiki wa Yanga na wa simba, ambapo Yanga waliwatandika watani wao bila huruma kwa mabao 2-0, huku Simba wakibaki kulalama ooh! nyie mnapiga mashuti mtamuumuzi golikipa wetu ooh sijui nini, yote hii haikusaidia kwani katika magoli yote walikaa madada, katika goli la Simba alikaa, Somoe Ng'itu na Yanga, alikaa Jenny John, huku muda wote akiutumia kusoma gazeti golini kutokana na ukuta wa ukweli uliokuwa mbele yake.
Na Mwandisi Wetu, jijini Dar es Salaam
Kampuni ya Bia Tanzania-TBL imeandaa semina ya siku moja kwa waandishi wa habari za michezo zaidi ya 50 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Semina hiyo inahusu namna ya kuripoti habari za mashindano ya Kili Taifa Cup 2010 yaliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Semina hiyo inawahusisha waandishi wa magazeti, redio,televisheni pamoja na Blogu.
Seminina hiyo inafanyika leo hii Aprili 14, 2010, kwenye Hoteli ya South Beach iliyopo Kigamboni.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja, semina hiyo inawasaidia waandishi wa habari kupata ujuzi zaidi katika kuripoti mashindano hayo ya Kili Taifa Cup na vile vile kuwa na wigo mpana wa masuala mengine ya soka.
Minja alisema, waandishi katika semina hiyo watapata mafunzo thabiti yatakayoratibiwa na kamati ya ufundi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
“Semina inapambwa na masuala mbalimbali kama vile mechi ambayo itajenga moyo wa ushindani baina ya vyombo vya habari,” alisema Minja.
Naye Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe amesema, TBL imekuwa ikiendesha semina kama hizo tangu ilipoanza kudhamini mashindano hayo ya kimataifa miaka minne iliyopita.
“Huu ni mwaka wa pili mfululizo tangu Bia ya Kilimanjaro ambayo ni moja ya bidhaa ya TBL, idhamini mashindano hayo ambayo yamesaidia kuibua vipaji vipya kutoka ngazi ya chini hadi timu ya taifa na katika klabu mbalimbali za soka ndani na nje ya nchi. Hata hivyo, huu ni mwaka wa nne kwa TBL kudhamini michuano hiyo,” alisema Kavishe.
Mashindano ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu ya ‘Kuipeleka soka ya Tanzania Kilele cha Mafanikio’ na yatashirikisha timu 24 zitakazocheza katika vituo sita na michuano inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 8, 2010 hadi Mei 15. Fainali za mashindano hayo yatafanyika jijini Dar es Salaam.
Vituo vya mashindano hayo ni Mtwara, Arusha, Dodoma, Tanga, Iringa na Shinyanga.
Udhamini wa mashindano hayo umegharimu Sh milioni 850 na kila timu itapata fedha kwa ajili ya maandalizi, usafiri, malazi na vifaa vya michezo.
Kwa muda mrefu, TBL imekuwa ikijihusisha na soka na daima imekuwa ikifurahia kudhamini katika eneo hilo.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ni watengenezaji na wauzaji wa bia, vinywaji vya matunda vyenye asili ya kilevi (AFB’s) na visivyo na kilevi ndani ya Tanzania. TBL inazo hisa pia katika Tanzania Distilleries Limited na kampuni shirika, Mountainside Farms Limited.
Bia maarufu za TBL ni pamoja na Safari, Kilimanjaro, Ndovu Special Malt na Castle. Vinywaji vingine vya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redds Premium Cold.
TBL imo pia katika Soko la Hisa la Dar es Salaam na imeajiri watu kiasi cha 1,300 huku ikiwa na wawakilishi katika sehemu kubwa ya Tanzania na viwanda vitatu vya bia na depot nane kwa ajili ya kusambazia bia na vinywaji vingine vya kampuni hiyo.
kwa maelezo zaidi wasiliana na:
George Kavishe,
TBL, Kili Brand Manager,
+255 767 266786
+255 767 266786,
george.kavishe@tz.sabmiller.com
Michael Mukunza,
Exective Solutions Limited,
+255 784 978302,
mikemukunza@gmail.com
or
m.mukunza@executivesolutions.co.tz

No comments:
Post a Comment