Habari za Punde

*BALOZI WA SWEDEN NCHINI ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA VITA VYA MAJIMAJI

Chifu msaidizi wa mkoani Songea, Aidan Mbano, akimkabidhi Barozi wa Sweden nchini, Staffan Herrstrom, zawdi ya Shoka la asili alipotembelea Makumbusho ya Taifa ya Vita vya Majimaji muda mfupi kabla ya kuzindua Mradi wa SPW unaoelimisha vijana kuhusu elimu ya ukimwi na elimu ya Uzazi inayoendana na kauli mbiu ya Kijana ni Afya.

Balozi wa Sweden nchini, Staffan Herrstrom, akionyesha Albam ya picha yenye nembo ya Ramani ya Tanzania iliyotengenezwa kiasili wakati alipotembelea Makaumbusho ya Taifa ya Vita vya Majimaji mjini Songea Mkoani Ruvuma jana, muda mfupi kabla ya kuzindua mradi ya SPW (Kijana ni Afya).

Wafanyakazi wa Mradi wa kuelimisha vijana kuhusu elimu ya uzazi na HIV wa SPW wakimuonyesha Balozi wa Sweden nchni, Staffan Herrstrom, takwimu jinsi wanavyofanya kazi ya kuelimisha kabla ya uzinduzi wa mradi huo katika Mkoa wa Ruvuma jana.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.