
Mwanamuziki kutoka Jamaica, Sean Kingston, akishambulia jukwaa, wakati wa onyesho lake lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam jana, kwa kushirikiana na wasanii waliopata tuzo za Kili Music Awards.

Kingston, akiendelea kukamua masong yake ambayo wabongo hawakuweza kupagawa nayo kama ambavyo walipagawa na masong ya wasanii wa Bongo.

Mwanamuziki kutoka Jamaica, Sean Kingston, akishambulia jukwaa, wakati wa onyesho lake lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam jana, kwa kushirikiana na wasanii waliopata tuzo za Kili Music Awards.

Hawa ni baadhi ya mashabiki waliokuwa wakimshangilia zaidi Kingston so, sijui ni sababu walikuwa ni wazungu ama la, kwani wabongo waliokuwa wakimshangili ni baadhi tu, tofauti na walipokuwa wakipanda wasanii wa Bongo.
"Ha ha habari ndo hiyo, Haha ha habari ndoyo hiyo"

Mchiz AY, akikamua song lake la Habari ndo hiyo jukwaani na kuwateka mashabiki.

Msanii wa kimataifa, Ambwene Yesaya (AY kushoto) na Hamis Mwinjuma (Mwana FA ) wakishambulia jukwaa.
"Tatizo kwetu Magalaaah!"

Hawa ni baadhi tu kati ya mashabiki lukuki waliojitokeza katika ukumbi wa Diamond Jubilee, kushuhudia onyesho hilo, wakipagawa na masong ya wasanii wa Bongo.

C-Pwaa, akipeana hi na mashabiki wake wakati alipokuwa akishambulia jukwaa.
Kiongozi wa kundi la Taarab la Jahazi, Mzee Yusuph, akiimba na kucheza na wanenguaji wake wakati wa onyesho la msanii wa muziki kutoka nchini Jamaica, Sean Kingston, lililofanywa kwa pamoja na wasanii walioibuka na tuzo za Kilimanjaro Music Awards, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam jana.

Msanii wa miondoko ya Hip Hop kutoka Kanda ya Kaskazini, Joe Makini, akishambulia jukwaa wakati wa onyesho hilo.
No comments:
Post a Comment