
Dk. Chain akiandaa mitambo kwa ajili ya kuonyesha Filamu hiyo mpya na ya kutisha, ama kwa hakika ni filamu ya kwanza Tanzania iliyoweza kurekodiwa na kuchanganywa, na kuhaririwa kwa hali ya juu huku ikitumia Effect ambazo hazijawahi kutumika na filamu zote za kutisha zilizokwishapita katika jukwaa la filamu za kutisha nchini.

Baadhi ya wasanii wakongwe pia walikuwapo katika hafla hiyo.

Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhulia hafla hiyo ya kyhakiki filamu hiyo katika ukumbi wa GRM, uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam jana.

Hata waha pia walikuwapo, ni Mama Dotinatha na Mumewe wakiwa pamoja na wageni waalikwa.

Filamu hii ilianza kwa mitego ya mdogo wa mkewe Alex (Dk. Chain), aliyekuwa akimtamani kwa muda mrefu shemejie, bila kujua kuwa huyo anayemtamani pia ni kiwembe asiyetaniwa na anayependa mambo fulani kupindukia, endeleaaaaaaa..................
"Dk. Chain alipofumaniwa na mkewe wakati akijivinjali na shemejie live bila chenga"
Dk. Chain akiwa katika chumba na kitanda anacholala na mkewe, tena akiwa na mdogo wa mkewe, Ebwana eeh, huyu 'Alex' katika filamu hii alikuwa ni wa ajabu kuliko na asiyemuogopa mtu kwani alikuwa na uwezo wa kufanya lolote alitakalo na kwa mtu yeyote amtakaye.

Kutokana na mdogo wa mkewe kumzimia Dk. Chain, alitumia kila njia kutaka kumkosanisha Chain na mkewe yaana dada yake, hapa aliingia ghafla na kuwakuta wamejipumzisha sebuleni, na huku akiongea na simu na kumpa shemejie akiigiza kuongea na jidume eti linalomchukua dada yake tena mbaye alikuwa ni mjamzito.

Dk. Chain 'Alex' alihamaki kusikia sauti ya jidume likiongea na kusisitiza kuwa eti ujauzito alionao mkewe ni wake, kilichofuata Chain alimtimua mkewe, nahisi unahisi kilichofuata kati ya Chain na shemejie kwani mkewe aliondoka na kumuacha mdogo wake kwa mumewe......

Alifika kwa Shangazi yake na kumueleza kilichomsibu hadi kurejea akiwa na mizigo yake.

Kazini kwa alex nako kulikuwa kukiwaka moto huku wengine wakiitaka nafasi ya Chain, hivyo iliwalazimu kwenda kwa waganga.

Huyu ni mmoja kati ya mabinti waliokuwa wakitakiwa na Alex, ambao walikuwa wakikiona cha moto usiku kwani ilikuwa ni nzozi za ajabu ajabu.......

Baada ya kumfumania mumewe akiwa na mdogo wake live ilikuwa ni mawazo na kilio kisichoisha......

Baada ya wafanyakazi wenzake Alex kwenda kwa mganga, Alex alikamatwa na kuhojiwa katika kituo cha polisi..lakini........

Umbea nao haukosekani katika hili.............

Alex hakuisha kwenda makaburini kumtaka ushauri bibi yake aliyemrisisha uchawi huo kabla ya kufariki, kila alipoona mambo magumu............

Huyu ni mmoja kati ya wale waliokuwa wakinyanyaswa na Alex kwa kuwataka wake zao kinguvu na kimiujiza, hapa walikuwa wakijiburudisha baa na ghafla......

Mzimu wa bibi wa Alex, ukimwelekeza na kumjulisha maadui zake.....

Alex baada ya kupigwa mshale na binti huku alex akijinaniliu......

Hatimaye binti aliyekuwa akisumbuliwa na Alex kila muda, alichukua jukumu la kumuua Alex, lakini alikufa yeye..........

Alex akionyeshwa na bibi yake kimiujiza wale wote wanaomfuatilia na kutaka kumuangamiza...

Katika filamu hii pia familia bora hazikukosekana, upendo wa namna hii kwa mwanao eeeeheeeee!

Mwisho wa yote Alex alifanikiwa kutimoza jina la filamu yake yaano mmoja baada ya mwingine, aliwaua wote hapa akipambana na.......

Baada ya kuua familia ya mshikaji, naye alimsimika panga la tumbo lililotokea upande wapili, lakini........

Jamaa anainuka na kurivenji.........

Panga la shingo.......duh!....................

Hawa ni baadhi ya washiriki katika filamu hiyo wakiwa ukumbini hapo wakati wa kuhakiki filamu hiyo.

Wasanii maarufu pia walikuwapo kumpa tafu mshkaji.

Hawa ni baadhi tu ya watu waliofanya kazi kubwa katika kuandaa filamu hiyo itakayokuwa na Party one na two.
No comments:
Post a Comment