Habari za Punde

*WAREMBO WA USTAWI NA UONGOZI MPYA WA CHUO HICHO WAPONGEZWA KWA BONGE LA PARTY

Kiongozi wa wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, aliyetambulika kwa jina moja la Landa naniliu, akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa hafla ya kuwapongeza warembo wa Chuo hicho walioingia katika nafasi tano bora kwenye mashindano ya Dar Inter College, yaliyomalizika hivi karibuni, ambapo sherehe hiyo pia ilikuwa ni Two in One kwani pia likuwa imeunganishwa na ile ya kuwapongeza Viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni katika Serikali ya Chuo hicho na kuwaaga wale waliomaliza muda wao. Party hiyo ilifanyika jana kwenye Ukumbi wa Hoteli mpya ya Dar City View iliyopo Mbezi juu jijini Dar es salaam.

Baada ya ufunguzi huo kilichofuata ilikuwa ni sebene za kufa mtu pamoja na magoma ya South yaliyowapagawisha vilivyo wanafunzi hao.

Haya twende sasaaaaaaaaaaaa!, mwenye nguo ya bule si mwingine ndiye aliyekuwa mshereheshaji wa sherehe hiyo ambaye hakuweza kuvulimia misebene iliyokuwa ikipigwa ukumbini hapo, na kuamua kuweka maiki pembeni na kuingia kati......

"Ebwana eeh pamoja na kucheza nawe lakini siku nyingi nilikuwa nakunanilu......bwana naomba unifikiliea m2 wangu"
Hapa walikuwa wakicheza tuuuuuu hadi mwisho.

Kila mtu alikuwa na patna wake.....

Gerald Simbeya (katikati) ambaye ni rais mpya wa Chuo hicho aliyechaguliwa hivi majuzi akiwa na baadhi ya viongozi wenzake ukumbini hapo.
"Twende tukaserebuke mtu wangu"
Hapa walikuwa wakichaguana kwa ajili ya kuingia kati kusakata rhumba, hajalishi umbo wala kimo, kama unavyochek hapa mdada huyo lakini kaka huyu kama mie............

"Jamani twendeni nasi tukacheze basi jamani"
Wengine walikuwa wakipata viburudishi tu huku wakiona aibu na kuogopa kamera la Sufianimafoto.

Warembo wakiserebuka.

Sebeneeeeeeeeeeeee!

Ni kujimwaga tu kwenda mbele.............

Warembo walikuwapo wa ukweli ukumbini hapo lakini........

Miss Dar Inter College 2010, Rose John (kushoto) akiserebuka na wenzake.

Warembo wa Ustawi bwana wanapenda sebene la South, lilipopigwa tu kila mtu alinyanyuka kwenye kiti na kuingia kati kucheza.

Hebu wacheki hapa utazani wanadarasa la kujifunza staili hii kwa pamoja.

Si unawacheki hapa hakuna mvivu wote ni staili moja tu hadi mwisho.......

Si kwamba wanalima la hasha! ni staili ya wimbo wa Amanda......

wengine utazani wanananiliu..........

Hawa pia walikuwa na kazi kubwa ukumbini hapo kuhakikisha wanaizitendea haki nyimbo zote zilizopigwa ukumbini hapo.

Hata Kaka dhao walikuwepo..........

Ebwana eeeh! hili ilikuwa ni miondoko ya alaji alaji alaji.........

Na hii si taarabu bali ilikuwa ni miondoko hiyo hiyo.......

Kamati ya maandalizi ya hafla hiyo haikuweza kuwaangusha wanafunzi hao kwani pia iliwaalika wasanii hawa wa kundi zima la Richard Mavoko 'Allow', ili kutoa burudani ukumbini hapo kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.......

"Heeeee! huyu mutu mbona anatukamapa mafotoo, acha weweeee utaharibu pozi"
Papaa akiserebuka na mrembo......

Kundi la Richard Mavoko, likishambulia jukwaaa......

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Richard Mavoko, akishambulia jukwaa na wanenguaji wake.

























No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.