Habari za Punde

*IGP MWEMA ZIARANI MKOA WA RUVUMA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Saidi Mwema, akiwasili kwenye Uwanja cha ndege cha mjini Songea Mkoani Ruvuma kwa ziara ya wiki moja. Picha Zote na Hassan Mndeme- wa Jeshi la Polisi.
Wasanii wa kikundi cha Sanaa cha Polisi jamii kutoka Bombambili Wilayani Songea, wakiigiza kama mgambo wa Jiji wakimkamata mama lishe, ikiwa ni sehemu ya burudani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Saidi Mwema, baada ya kuwasili mkoani Songea kwa ajili ya kuzindua kitabu cha ‘Haki na Wajibu wa Mpiga Kura’ wakati wa ziara ya wiki moja mkoani humo.

IGP Mwema akisoma hotuba yake wakati akizindua Kitabu cha 'Haki na Wajibu wa Mpiga Kura ' Mkoani Ruvuma kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao chenye lengo la kuwaelimisha wananchi mambo ya msingi wakati wa zoezi la uchaguzi.
IGP Mwema, akikabidhi sehemu ya msaada kwa wananchi




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.