Mchezaji aliyetokea timu ya African Lyon, Robert Sentongo, leo ameiwezesha timu ya simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 baada na kufungua mlango wa magoli kwa kuifungi timu yake bao la kwanza katika dakika ya 30 ya kipindi cha kwanza na kuifanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa kifua mbele kwa bao 1-0.
Kiipindi cha pili Atraco iliweza kusawazisha goli hilo kupiti mchzaji wake Kadogo Almas, katika dakika ya 68 na katika dakika ya 89 ya mchezo Simba iliweza kupata penati na mpira ukawekwa Kimiani na Mussa Hassan Mgosi, hivyo hadi mpira unamalizika Simba imeibuka kidedea kwa kutoka kifua mbele kwa mabao 2-1.
No comments:
Post a Comment