Habari za Punde

*LUKUVI AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MACHINGA COMPLEX, LEO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi (katikati) akikagua jengo la biashara la Machinga Complex, wakati wa ziara yake leo kukagua maendeleo ya ujenzi na ukamilishwaji wa jengo hilo. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Machinga, Mseli Abdallah (kushoto) ni Msanifu Majengo Mkuu, Eric Ibrahim. Lukuvi amewataka wasimamizi wa ujenzi huo kuwa wamekamilisha na kuwakabidhi wafanyabiashara wadogo Machinga ifikapi Juni 20 na tayari wawe wameshaanza kufanya biashara ili badala ya kwenda tena kukagua jengo hilo bila watu wala biashara iwe ni kukagua jengo likiwa limekamilika na likiwa linatumika kama ilivyopangwa.

Lukuvi akiendelea kutembezwa katika maeneo ya jengo hilo, hapa ni moja kati ya maeneo ya kufanyia biashara 'viota'.

"Ahaaa! kumbe tayari yanatoa hadi huku juu ni ghorofa ya mwisho hapa siyo?
Lukuvi akikagua eneo la chooni katika masinki ya maja kama maji hayo tayari yamekwishaanza kutoka ama la.

Lukuvi, akiwa ndani ya kiota cha kufanyia biashara watakachopewa wamachinga hao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.