Baadhi ya Wasanii wanaounda kundi la Makhilikhili, wakionyesha vionjo vyao wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusiana na maonyesho yao wanayotarajia kufanya hapa nchini, baada ya kuwasili jana. Kiongozi wa kundi hilo la Dansi ya asili kutoka Botswana la Makhilikhili, Moses Malapela ‘Shumba Ratshega’, aliyefika nchini na kundi lake kwa ajili ya maonyesho kadhaa, alitoa tafsiri ta neno MAKHILIKHILI kuwa ni mwanaume ama mwanamke anayetoka nje ya ndoa yake yaani kuisaliti ndoa na kupenda kufanya mapenzi nje ya ndoa yake, ambapo alisema kuwa neno hilo kwa nchini kwao linatumika kikawaida kabisa japo linaoshesha kuwa ni 'matusi' lakini linatumika namna hiyo ili kuweza kufikisha ujumbe kutokana na hali mbaya ya maambukizi ya Ukimwi nchini kwao. Tigo ni miongoni mwa wadhamini wa ujio wa kundi hilo.
NAIBU WAZIRI KIHENZILE ATEMBELEA BANDA LA TCAA MKUTANO WA 18 WA PAMOJA WA
MAPITIO YA SEKTA YA USAFIRISHAJI
-
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile, Disemba 15, 2025
ametembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika
Mkutano wa 18 wa...
51 minutes ago
No comments:
Post a Comment