Menu

Wednesday, May 26, 2010

*MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA LEO

*WAKAZI WA MALAGARASI WAKOSA NJIA, WAVUKA KATIKA DARAJA LA TRENI
Wanawake hawa wakazi wa maeneo ya karibu kabisa na daraja la Malagarasi, wakivuka na baiskeli zao katika daraja hili kupitia katika njia ya Treni, bila kuogopa kukutana na treni au kutereza na kudondoka katika mto wa daraja hilo ambao huvuka kutoka ng'ambo upande wa Nguruka wakielekea Uvinza kutafuta mahitaji ikiwa na umbali mrefu, kufutia njia ya barabara iliyokuwa ikitumika kuharibika na kujifunga kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kufanya mto huo kumwaga maji yake nje ya mkondo wake wa jambo lililochangia usafiri kati ya pande hizo kuwa mgumu. Picha na Iddi Risasi
*BARABARA ZA JIJI LA LUKUVI SASA NI HATARI TUPU
Hii ni barabara ya Uhuru karibu kabisa na Shule ya Benjamini Mkapa, iliyopo Shule ya Uhuru jijini Dar es Salaam ikiwa imeharibika vibaya kiasi cha kuifanya barabara hiyo kuwa finyu kutokana na mvua zinazoendele kunyesha jijini. Wahusika wanatakiwa kuzifanyia ukarabati wa haraka barabara hizo ili kuepusha usumbufu na msongamano wa magari usio wa lazima.

*HUKU NI KUFULIA AU NDIYO KILA KITU KINAKWENDA KIJELA JELA?
Ebwana mie sikuweza kuamini kama Pingu ingeweza kufanya shughuli mbili kwa wakati mmoja, yaani kufungia watuhumiwa na kufungia mageti, kama inavyoonekana PINGU, hii ikiwa imefungiwa geti la nyuma la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam badala ya kufuli, eti jamani hii ni sawa?
*MSUKUMA MKOKOTENI ATUNISHIANA MSURI NA DALADALA.
Msukuma mkokoteni, ambaye hakuweza kufahamika jina lake, akipeana pande na daladala katika mtaa wa Uhuru Dar es salam leo, wakati dereva wa gari hilo alipokuwa akitaka kutoka nje ya barabara hiyo ya Uhuru ili kukwepa foleni na gari lililokuwa 'linadilay' mbele yake bila kupita, bila kutazama site millar, dereva huyo alitoa gari na kuuvaa mkokoteni huo huku dereva wa mkokoteni akibaki kipiga kelele ya kuzuia gari hilo lisiendelee kuelekea upande wake.





No comments:

Post a Comment