WANANCHI wenye hasira kali wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtanzania limeshuhudia.
Kijana huyo mkazi wa Mwanza anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, alianguka jana saa 12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa alikuwa kwenye safari zake za kishirikina.
Kabla ya kufariki alisema “mimi nilikuwa na wenzangu sita, wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu”
“Lakini mimi kwa bahati mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa kufungua macho ndipo ghafla nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea mauti yangu”
Hata hivyo kutokana na vurugu zilizokuwapo eneo
Kwa mujibu wa mashuhuda wengine wa tukio
“Huyu jamaa bwana, ameanguka hapa, sasa kwakuwa sisi hatuna mzaha na watu
Hata hivyo baadhi ya wananchi walielekeza lawama zao kwa Jeshi la Polisi (Kituo cha Polisi Kimara) kilichopo Mbezi kwa Yusuph kwa kuchelewa kuja kumuokoa kija huyo ingawa walipewa taarifa mapema.
“Sisi tumepiga simu kituoni hapo hata kabla huyu mchawi hajaanza kushambuliwa, lakini angalia tukio limeanza saa 12 asubuhi wanakuja baada ya masaa mawili, huu nu uzembe” alisema mkazi wa eneo
Ingawa katika tukioa
Mtanzania lilibisha hodi katika kituo cha Polisi Kimara ambacho mwili wake ulipelekwa ili kupata uthibitisho zaidi lakini askari wa zamu waliokuwa mapokezi walisema hawana mamlaka ya kutoa maelezo hadi mkuu wa kituoa au mkuu wa makosa ya kieupelezi wa kituo hicho ndiyo wenye dhamana.
Aidha wakuu hao OC CID (ASP) M. Mganga pamoja na Mkuu wa kituo wote hawakuwapo kituoni wakati Kamanda wa kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga hakuweza kupatikana ili kudhibitisha tukio
No comments:
Post a Comment