Habari za Punde

*MGOGORO WA ARDHI WANUKIA MBEZI JUU, WANANCHI WAJIKATIA MAENEO

*Mwenyekiti ajichukuliwa 'madaraka' auza maeneo kinyemelaMwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mtoni Mbezi Juu jijini Dar es Salaam, aliyetambulika kwa jina moja la Jose (kulia) akiwaonyesha wateja wake ambao walifika kwa lengo la kuonyeshwa maeneo ili kununua. Pia msingi huo unaoonekana pichani ni jengo hilo ni msingi unaoelezwa kuwa umejengwa na Mwenyekiti huyo akidai ni Hospitali ya milioni 20 kama ilivyokuwa imeamuliwa na wanakijiji, angalizo ni kwamba baadaye asije kuwageuka tu na kuwaambia kuwa alikuwa akijenga frem zake za biashara hali ya kuwa pesa anazotumia ni kati ya alizouza viwanja hivyo.
"TUNACHUKUA CHETU MAPEMA". Vijana wa Mbezi Juu kwa Sanya jijini Dar es Salaam, wakijipimia maeneo ili kujimikisha baada ya Mwenyekiti wao wa serikali ya mtaa, ambaye imeelezwa amekuwa akijichukulia maamuzi binafsi na kuuza maeneo hayo bila kuwashirikisha wananchi, hali ya kuwa eneo hilo lilikwisha tengwa na wanakijiji hao kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali na mambo mengine ya Maendeleo.
Vijana hao wakiendelea na zoezi la kujipimia maeneo hayo.

"Wacha na mie nijisevie kijieneo hiki"
Huyu si kijana lakini pia naye aliamua kujikatia kijieneo na kufyeka ili aweke alama zake ili nae awe tayari ameshatwa chake mapema.

Baadhi ya watendaji katika Kamati ya Maendeleo iliyoteuliwa na Wananchi wa maeneo hayo, wakiwapimia maeneo wananchi waliokuwa tayari kulipa fedha ili kupewa maeneo hayo wakiwa na ndoto za kuendelea na malengo waliyopanga kuyafikia, wao wakiwa na imani hii, Mwenyekiti wao nae akifikilia jinsi ya kuwazidi kete "PATAM HAPO".

Ebwana eeh! zoezi linaendelea.






No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.