Habari za Punde

*MWEKEZAJI HIDARY ACHANGIA MIFUKO 100 UJENZI WA SHULE

Kutoka (kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Magesa Mulongo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Fukayosi, Salum Mkecha, Mtendaji wa Kijiji, na Mwekezaji Hassan Hidary, wakipiga picha mbele ya roli lenye mifuko 100 ya Cement iliyotolewa na mwekezaji huyo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule ya Msingi Mtakuja iliyopo katika Kijiji hicho ikiwa ni sehemu ya Irani ya Serikali na imani ya wapenda maendeleo kuchangia Elimu nchini.


Mkuu wa Wialaya ya Bagamoyo, Magesa Mulongo (kulia) akipokea sehemu ya msaada wa mifuko ya Cement 100, kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Rendis Transport Ltd, Hassan Hidary, kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule ya Msingi ya Mtakuja iliyopo Kata ya Kiwangwa, Tarafa ya Msata Kijiji cha Fukayosi, wilayani humo, wakati wa makadhiano hayo yaliyofanyika kijijini hapo jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Salum Mkecha.

Mwekezaji Hidary, akizungumza machache mbele ya wanakijiji waliohudhulia hafla hiyo kabla ya zoezi la kukabidhi msaada huo.

Hidary akimwaga sera.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Magesa Mulongo, akizungumza na waandishi wa habari na wanakijiji wa Fukayose, kabla ya kukabidhiwa msaada huo, ambapo Magesa aliwaasa wanakijiji hao kuheshimu msaada huo kwa kuutumia katika malengo yaliyokusudiwa.





No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.