Na Sufianimafoto Reporter, jijini Dar es Salaam
MWANAMUZIKI mahiri wa kutoka nchini Jamaica, Sean Kingstone, amewasili nchini juzi usiku akiwa na kundi lake la watu 13, ambao ni sehemu ya bendi yake itakayofanya onyesho jijini Dar es Salaam kesho katika ukumbi wa Diamond Jubilee katika onyesho la washindi wa Kilimanjaro Tanzania Music Awards.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, alisema kuwa kingstone anatarajia pia kufanya mahojiano katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni, pamoja na kujiandaa na utoaji wa zawadi kwa washindi wa Kilimanjaro Music Awards katika hafla hiyo itakayofanyika leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Aidha alisema kuwa onyesho kamili la Kingstone linataraji kufanyika kesho, ambapo pia atakuwa akiwasindikiza washindi wa Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2010, ijulikanayo kama ‘Winners Concert’.
Mwanamuziki huyo aliyezaliwa miaka 20 iliyopita katika mji wa Frolida marekani, anatamba zaidi na vibao vya Beautiful Girls, Me Love, Take you There, There’s Nothin aliomshirikisha Paula DeAnda, Gotta Move Faster, Fire Burning na Face Drop.
Pia mwanamuziki huyo alishawahi kujinyakulia tuzo mbalimbali katika ulimwengu wa muziki ambapo 2008, alipata tuzo ya Outstanding New Artist ‘Nominated’ mwaka 2007 alipata tuzo za Best Reggae Acts, Choice R&B Track ‘Beautifull Girls’, Choice Summer Track ‘Beautifull Girls’ na 2009, akajinyakulia tuzo ya Choice Summer Song ‘Fire Burning’.
No comments:
Post a Comment