Menu

Saturday, May 15, 2010

*TUZO ZA KILI 'MUSIC AWARDS' DIAMOND ANG'ARA

Kutoka kung'ara katika fani ya urembo hadi kufanya kweli katika jukwaa la muziki wa Kizazi kipya, ni Jokate Mwegelo, akiimba jukwaani na AY, wakati wa hafla ya Kili Music Awards, iliyofanyika jana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.
"Unashangaa nini weweeee? hiki ndo kivazi cha mamtoni we chezea simu tu"
Mdada huyu aliacha shughuli zote alizokuwa akifanya katika simu yake na kumshangaa mwanadada, msanii wa muziki wa kizazi kipya tena anayetokea katika familia ya kimuziki, Maunda Zorro, wakati akiingia ukumbini humo huku akisalimiana na kila mtu na kuwaacha hoi baadhi ya watu waliokuwamo ukumbini humo.

Huyu simu mwingine ni msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya, Diamond, akipozi na Mama yake mzazi baada ya kujinyakulia jumla ya tuzo tatu, akiwa kama msanii bora chipukizi na wimbo bora, wakati wa hafla hiyo jan.

Mkurugenzi wa Kituo cha Radio cha Clouds Fm Intertaiment, Ruge Mutahaba, akiwa na Tunzo ya Kituo hicho ya baada ya kukabidhiwa kwa kuwa kituo bora kinachopiga nyimbo za wasanii mara nyingi tofauti na vituo vingine.






No comments:

Post a Comment