MTU WA KWANZA ILIKUWA NI SAA 9:00 ASUBUHI
akimkabidhi Fomu ya kuwania nafasi ya Urais Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, wakati alipofika
kuchukua fomu hizo kwenye ofisi hizo mjini Zanzibar jana.
MTU WA PILI ILIKUWA NI SAA 10:00 ASUBUHI
akimkabidhi Fomu ya kuwania nafasi ya Urais Zanzibar, Ali Abeid Karume, wakati alipofika
kuchukua fomu hizo kwenye ofisi hizo zilizopo Kisiwandui mjini Zanzibar jana. Kulia ni Mkewe, Hudda Ali.
kumsindikiza wakati wa kuchukua fomu.
MTU WA TATU ALICHUKUA SAA 11:00 ASUBUHI
akimkabidhi Fomu ya kuwania nafasi ya Urais Zanzibar, Ali Juma Shamhuna, wakati alipofika
kuchukua fomu hizo kwenye ofisi hizo mjini Zanzibar jana.
MTU WA NNE ALICHUKUA SAA 12:00 MCHANA
Baadhi ya wananchi wakiwa nje ya Ofisi za CCM Makao Makuu Kisiwandui mjini Zanzibar, wakimsubiri, Hamad Bakari Mshindo, wakati alipokuwa akija kuchukua fomu.alipofika kuchukua fomu hizo kwenye ofisi hizo mjini Zanzibar jana, na baadaye alifanya mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo mjini humo na baada ya hapo ilikuwa ni mapumziko ya saa moja kabla ya mtu wa tano.
MTU WA TANO ALICHUKUA SAA 2:00 MCHANA
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Makao makuu ya Ofisi ya CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai (kushoto)akimkabidhi Fomu ya kuwania nafasi ya Urais Zanzibar, Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar,Mohamed Gharib Bilali, wakati alipofika kuchukua fomu hizo kwenye ofisi hizo mjini Zanzibar
jana, naye baada ya hapo alikutana na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Zanzibar Ocean View na kufanyanao mkutano.
HATIMAYE ALIKUA NI DK. SHEIN MTU WA SITA SAA 3:00 MCHANA
Huu ulikuwa ni msafara wa magari ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk, Ali Mohamed Shein, alipokuwa akiingia katika viwanja vya Ofisi hizo.
Baadhi ya wapambe wa Dk Shein wakiwa nje ya ofisi hizo, wakimsubiri.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na wananchi nnje ya Ofisi za CCM Makao Makuu Zanzibar, kabla ya kuingia kuchukua fomu zakugombea nafasi ya Urais Zanzibar.
Dk. Shein, akiwa na baadhi ya waumini wa dini ya kiislam, wakiomba dua katika kaburi laaliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Abeid Aman Karume, lililopo nje ya ofisi hizo zilizopo
Kisiwandui.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Makao makuu ya Ofisi ya CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai (kushoto)akimkabidhi Fomu ya kuwania nafasi ya Urais Zanzibar, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Ali Mohamed Shein, wakati alipofika kuchukua fomu kwenye ofisi hizo mjini Zanzibar jana.
baadhi ya wazee na Dk. Shein wakiomba dua baada ya kukabidhiwa fomu.
Dk. Shein, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar baada ya kuchukua fomu jana.WA MWISHO ALIKUWA NI MOHAMED ABOUD ALICHUKUA SAA 4:00
Mke wa Mohamed Aboud Mohamed, akikabidhi fedha Sh. Milioni 1 kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Makao makuu ya Ofisi ya CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
Mke wa Mohamed Aboud Mohamed, akikabidhi fedha Sh. Milioni 1 kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Makao makuu ya Ofisi ya CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai.

No comments:
Post a Comment