Habari za Punde

*MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA JIJINI DAR LEO

TIGO YAKABIDHI ZAWADI ZA PROMOSHENI YA 'JIKOKI NA TIGO'
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu za mkononi, Tigo, Jackson Mmbando (kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa Promosheni wa ‘JIKOKI NA TIGO’, Alfonsina Ladislaus, aliyejishindia kitita cha Sh. Milioni 2, Simu aina ya Brack Berry na Lap Top, katika droo ya kwanza ya Promosheni hiyo. Washindi hao walikabidhiwa zawadi zao jijini Dar es Salaam leo.
'MTAFUTAJI HACHOKI'
Mwanamama mkazi wa jijini Dar es Salaam, akiwa na beseni lake la mihogo na machungwa akipita katika mita ya Posta jijini, kutafuta wateja, kama alivyonaswa na kamera ya sufianimafoto leo.

DEREVA WA BAJAI MDADA AKISUBIRI WATEJA KATIKA BAJAJI YAKE
Bajai hata madada zetu pia wamo, wenyewe wanasema riziki ni ilimradi tu mkono uende kinywani, Dada huyu akiwa kwenye Mtaa wa Samora Dar es Salaam leo mchana akisubiri wateja katika usafiri wake wa bajaji, sasa sijui huyu jamaa wa nyuma ni abiria ambaye alikuwa akisubiri usafiri huo ujae kama zinavyofanya daladala ama vipi.....Kazi kwenu madada...

MASHABIKI WA SOKA WAHAHA TFF KUSUBIRI TIKETI ZA TAIFA STARS NA BRAZIL
Baadhi ya mashabiki wa soka wakiucha usingizi nje ya ofisi za Shirikiso la Soka nchini TFF, wakati wakisubiri utaratibu wa kununua tiketi za kushuhudia Soka la Kirafiki baina ya Taifa Stars na Brazil, mchezo unaotarajia kuchezwa siku ya Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya mashabiki wa soka wakiwa kwenye Ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini kusubiri kununua tiketa za kushuhudia mchezo wa kirafiki baina ya timu ya Tanzani, Taifa Stars na Brazil, mchezo unaotarajia kuchezwa jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam

USINGIZI POPOTE, JAMAA AUCHAPA USINGIZI JUU YA MIZIGO, JUU YA GARI
Ebwana eeh! jamaa huyu sijui haogopi? hebu mcheki alivyouchapa usingizi juu ya mzigo lumbesa tena wakati gari hilo likiwa katika mwendo, kama alivyonaswa na kamera ya Sufianimafoto eneo la magomeni Mwembe Chai Dar es Salaam leo, Hatari tupu....
USINGIZI NI NOMA JAMANI UKIKUBANA UTAANGUSHA POPOTE HUNA UJANJA
Mkazi wa jijini Dar es Salaam akiwa ameuchapa usingizi pembezoni mwa barabara ya Morogoro eneo la Magomeni, jijini Dar es Salaam leo bila kujali usalama wake kutokana na njia hiyo kutumika na Pikipiki na Baiskeli.





No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.