Na Willy Sumia, Sumbawanga Wakazi wa manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wameiomba Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI kuangalia upya safu ya watendaji wa Manispaa hiyo kutokana na kile walichodaiwa kuwa ni mambo kutokwenda vyema.
Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Sumbawanga baadhi ya wakazi hao wameilalamikia Manispaa hiyo kuwa imekuwa ikifanya vibaya katika baadhi ya sekta hali inayopelekea kukosekana kwa baadhi ya huduma za jamii zitolewazo na taasisi hiyo.
walisema kuwa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka jana Manispaa ya Sumbawanga ilishika mkia katika matokeo hayo na kuifanya Manispaa hiyo kuwa ni Halmashauri iliyofanya vibaya katika mkoa wa Rukwa katika mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2009/2010.
walisema kuwa katika sekta ya miundombinu nako kumekuwa na matatizo ya kiutendaji kutokana na viwango duni vya ujenzi wa barabara zilizopo mjini Sumbawanga ambazo ilipelekea mkuu wa mkoa wa Rukwa kuunda tume yakuchunguza ubora wa ujenzi wa barabara hizo kwa kiwango cha lami pamoja nabarabara za vumbi zilizoko mjini Sumbawanga ambapo wananchi hao walitoa mfano vifusi vilivyoko katika barabara ya Msakila kuwa vimeachwa kwa zaidi ya miezi sita katika barabara hiyo hali inayoashiria kutelekezwa kwa barabara hiyo muhimu katika mji huo.
Aidha walilalamikia pia mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi ya mikoani katika mtaa wa jangwani ambapo wananchi hao walidai kuwa ujenzi wa kituo hicho cha mabasi kimechukua muda mrefu sana kukamilika na kuwa ujenzi wake umekuwa chini ya kiwango.
Pia walisema hukwa mji wa huo umekuwa ukitoaharufu nzito katika mitaa ya Jangwani kutokana na uozo na majitaka yaliyopo katika mifereji ya mji mahala hapo.
No comments:
Post a Comment