Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager wadhamini wakuu wa timu za Yanga na Simba za Jijini Dar es Salaam, zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, leo imekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya Sh. milioni 64
kwa timu hizo ikiwa ni sehemu ya udhamini wake kwa Klabu hizo kuelekea msimu wa Ligi Kuu unaotarajia kuanza mwezi ujao.
Meneja Uhusiano wa TBL Editha Mushi (katikati) akimkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa mpya wa Klabu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, Lloyd Nchunga, wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Klabu za Yanga na Simza iliyofanyika kwenye Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, (TFF) leo mchana. Kushoto ni Meneje wa Bia ya Kilimanjario George Kavishe na (kulia) ni katibu wa Klabu ya Yanga, Lawrance Mwalusako.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo, Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Geofrey Kaburu.
Mchezaji wa Yanga, Athuman Idd (Chuji) akijaribisha vifaa hivyo wakati wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment