Baada ya kumaliza ziara yake ya mkoa wa Lindi katika kuinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi, hatimaye Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, leo jioni amepokelewa kwa shangwe kubwa na wananchi wa Mkoa wa Mtwara na kuanza kuwahutubia wananchi hao katika mkutano wake wa kwanza katika mkoa huo kwenye Uwanja vya Mashujaa. Dk Bilal kesho anatarajia kuanza safari ya kuelekea Vijiji vya Mkoa huo kwa ajili ya kuinadi Ilani na kumuombea Kura Mgombea Urais Dk Jakaya Kikwete, Wabunge na Madiwani wanaowania nafasi hizo kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi.
Rekodi Mpya: TISEZA Yasajili Miradi 177 na Trilioni 2.9 Kumwagika Tanzania
-
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA)
imetangaza neema ya kiuchumi baada ya kusajili miradi 177 katika robo ya
kwanza ya...
6 hours ago
No comments:
Post a Comment