Habari za Punde

*MATOKEO YA KURA ZA MAONI PWANI


Na Mwandishi Wetu- Pwani
VUTA ni kuvute aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la kibaha mjini Dk. Zainabu Gama , imemlazimu kuandika barua ya kukata rufaa na kuipeleka katika ofisi ya katibu wa CCM mkoa wa Pwani ,kwa madai ya kuhujumiwa katika uchaguzi wa kura za maoni.
Dk.Zainabu Gama ambaye kwa sasa amebwagwa kwa kupata kura 1243, wakati Profesa Samwel Wangwe ,aliyeibuka na kura 2570 huku Silvester Koka,aliyeshinda kwa kura 4303 kumesababisha Jimbo la Kibaha mjini kujawa na ndelemo kubwa .

Aidha kwa mujibu wa Katibu wa CCM wa Mkoa wa Pwani ,Sauda Mpambalioto, alisema kuwa uchaguzi huo ulifanyika huku kukiwa na amani na utulivu katika majimbo yote tisa na changamoto zilizojitokeza zilirekebishwa kwa wakati.

Katika matokeo hayo jimbo la Mkuranga, mpaka sasa limeongozwa na Adamu Malima kwa kupata kura 5805, wakati Abdallah Ulega, ambaye ni mwenyekiti wa vijana wa mkoa wa Pwani amepata kura3763,Mbaraka Kihame(3437) wakati Rukia Msumi(630).

Kwa upande wa Jimbo la Kisarawe ,limeongozwa na Selemani Jafu ,kwa kura (5835),Omary Dibibi(1544),Ramadhani Maleta(768),Maneno Mbegu(418) ,na Ally Kano(1040),alikadhalika Jimbo la Mafia limeongozwa na Mbunge mtetezi Abdulkarim Shah(1846),Omary Kimbau(1794),Hafsa Khalfani(759),Jimbo la Bagamoyo Shukuru Kawambwa ameendelea kulitawala kwa kupata (6576),dhidi ya DK.kasambala aliyepata (1061),wakati huohuo Jimbo la Chalinze Saidi BwanaMdogo ameibuka kinara (6777 )na kumbwaga aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Ramadhani Maneno(3140) wakati Imani Madega akiambulia kura(3896).Jimbo la Kibiti Jabir Malombwa amekuwa kinara kwa kura 2840 na kumwangusha Kasongo pamoja na Kambangwa wakati Rufiji DK . Seif ameshinda kwa kura (2362)huku Mbunge mtetezi Idriss Mtulia, maji yamemfika shingoni kwa kuambulia(2042)na Mohamed Hafifu akiwa wa mwisho kwa kura(101).
Hata hivyo, Jimbo la kibaha Vijijini ,hali bado ni tete kwani mpaka sasa matokeo yake bado hayajatangazwa lakini kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari zilisema kuwa Dk. Ibrahimu Msabaha, yupo mashakani kubwagwa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.