
MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Nchinga(CCM) Mudhihiri Mudhiri amesema hana kinyongo kinyongo baada ya kubwagwa katika kura za maoni za chama Na hicho zilizomalizika hivi karibuni.
Mudhihiri aliyasema hayo jana wakati akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika wilaya ya Lindi Vijijini katika kijiji cha Kilangala, mkutano ulioudhuliwa pia na mgombea mwenza wa CCM-Dk.Ghalib Bilal,mkewe Asha Bilal na mgombea wa Jimbo la Nchinga, Said Mtande.
Mudhihiri amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa vipindi vitatu ambapo awali ilidaiwa kudondoshwa kwake kulitokana na kutoelewana kwake na Mbunge wa Mtama ambaye pia ni waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe.
“Sisi katika CCM hatuna tabu,hata kama kuna vita ndani yetu tunaimaliza baada ya uchaguzi…na kwasababu hiyo makundi yamekwisha kwahiyo natangaza rasmi kwa myo mmoja nitamuunga mkono mgombea ubunge wa sasa na nitaakikisha anapata ushindi wa kishindo”alisema Mudhiri huku akimalizia hotuba yake kwa kuimba wimbo.
Kwa upande wa Dk.Bilal akimnadi mbombea ubunge wa Nmbung huyo kwani mgombea huyo ni kijana, msomi na anayekifahamu chama na mwenye kiu ya kule maendeleo kwenye jimbo hilo.
Aidha Dk.Bilal aliomba alisisitiza kwa kuwataka wanachama wa chama hicho kumaliza makundi haraka iwezekanavyo kwani siku zote panapokuwepo makundi yanayohasimiana ndani ya chama ni wazi chama hicho kinaweza mara kwa mara kinaweza kujikuta kinaingia kwenye migogoro isiyonatija.
“Mmesikia Mudhihiri ,kasema wazi hapa jukwaani kwamba makundi kweli yalikuwepo ndani ya chama hapa wilayani lakini baada ya kula za maoni kumalizika makundi hayo wameyazika…hivyo nampongeza kwa hilo kwani ni wazi madiwani na mbunge wa ccm hapa watashindwa kwa kishindo kwasababu sasa wana CCM wamekuwa kitu kimoja”alisema Dk.Bilal ambaye leo anaendelea na ziara ya kampeni katika wilaya za mkoani hapa.

Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilali, akisalimiana na Mgombea wa Ubunge Jimbo la Mchinga, Said Mtanda na wakazi wa Kijiji cha Mkuwajuni baada ya kuwasili wilaya ya Lindi Vijijini leo mchana kwa ajili ya kuendelea na mikutano ya Kampeni, ambapo mkutano wa kwanza ulifanyika katika viwanja vya Tawi la Kilangala B, Wialaya ya Lindi Vijijini Mkoa wa Lindi.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mchinga, Said Mtanda na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Mudhihir Mudhihir, wakiteta jambo wakati walipokuwa kwenye mkutano wa Kampeni wa Mgombea Mwenza.
Mtoto wa kike akiwa na sinia la Bamia katikati ya Umati wa watu wakazi wa Kijiji cha Kilangala, waliokuwa kwenye mkutano wa Kampeni wa Mgombea Mwenza keo.
Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilali, akisalimiana na wakazi wa Kijiji cha Mkuwajuni baada ya kuwasili wilaya ya Lindi Vijijini leo kwa ajili ya kuendelea na mikutano ya Kampeni, ambapo mkutano wa kwanza ulifanyika katika viwanja vya Tawi la Kilangala B, Wialaya ya Lindi Vijijini Mkoa wa Lindi.
Mgombea Mwenza, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na kuagana na Viongozi wa Wi ilaya ya Kilwa, wakati alipokijijini leo katika ziara yake ya mikutano ya Kampeni.
Mke wa Mgombea Mwewnza, Asha Mohamed Gharib Bilal, akicheza pamoja na wasanii wa Kikundi cha Siasa Makondeko, aliposimama kuwatunza baada ya kufurahishwa na ujumbe wa wasanii hao, wakati wa mkutano wa Kampeni leo. 

No comments:
Post a Comment