Habari za Punde

*DK. BILALI AACHA GUMZO PWANI KATIKA KAMPENI

Na Sufianimafoto Reporter, Pwani

MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Bilali amesema ifikapo mwaka 2015 kila shule ya msingi kote nchini itapaswa kuwa na darasa moja la wa chekechea.

Dk.Bilali aliyasema hayo leo mchana wakati akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Rufiji katika mkutano wa adhara uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Mhoro Kata ya Chumbi mkoani Pwani sambamba na kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Rufiji Dk. Seif Rashid na mgombea ubunge wa Jimbo la KIbiti,Abdul Marombwa,alisema mpango huo mkakata umeainishwa katika Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015.

Dk.Bilali ambaye jana ndiyo alianza ziara ya kampeni yake rasmi mkoani hapa alisema lengo la mpango huo kuingizwa kwenye ilani hiyo ya CCM, ni chama hicho kupitia serikali yake inataka kuona wanafunzi wa shule wanaomaliza shule za awali wanajiunga na shule za msingi na sekondari na kisha kujiunga na vyuo vikuu.

“Hivi sasa taifa lisilo na wasomi ni dhahiri halitaweza kupiga hatua za kimaendeleo kwa wakati hivyo kwakuwa inapenda kuona wananchi wake wakubwa kwa wadogo wakipita elimu ndiyo maana ilani ya mwaka 2010-2015 imewekea mkazo suala la ukuzwaji wombea sekta ya elimu kwa ngazi zote hivyo nawasii sana wazazi na wananchi kote nchini muwaruhusu watoto wenu waende mashuleni kupata elimu kwani hakuna ulithi usiooza kama elimu.

Huku hotuba yake ikikatishwa mara kwa mara na vibwagizo vya nyimbo za kukisifu chama na kumpongeza rais Jakaya Kikwete kumchagua Dk.Bilali kuwa mgombea mwenza, alisema ili mpango huo utimie wananchi wa kada zote hawana budi kuinga mkono serikali ya ccm ilikuweza ujenzi huo wa madarasa ya wananfunzi wa shule za awali yanajengwa na kuongeza kwa kuwataka wananchi wote wanampatia kura za ndiyo mgombea urais wa ccm,Kikwete Leo mgombea mwenza ataendelea na ziara yake ya kampeni mkoani Kilwa.

Mtoto wa Shule ya Msingi Muhoro, akitoa mpya baada ya kukimbia kutoka shuleni kuwahi kumsikiliza Mgombea Mwenza na kuanza kukwepa mawe 'kuuchapa usingwai' huku akiwa na unifom na madaftari yake, Usingizi dawa bwana weee.....
Mkuu wa Wialaya ya Kilwa Masoko, Nurdin Babu, akiongozana na Mgombea Mwenza Mohamed Gharib Bilali, wakati alipompokea mpakani mwa Wilaya ya Rufiji kuingia kwenye Wilaya yake, kuendelea na mkutano wa Kampeni leo
Mgombea Mwenza, Mohamed Gharib Betiilali, akisalimiana na wakazi wa Somanga, mpakani mwa Wilaya ya Rufiji na Kilwa Masoko, wakati wakazi hao walipokuwa wakimpokea mgombea huyo aliyekuwa akiingia Wilaya hiyo kuendelea na mkutano wa Kampeni.

Umati wa watu, Wakazi wa Somanga wakimzunguka Mgombea Mwenza na kufunga barabara kwa muda ili kumpokea mgombea huyo alipokuwa akipita eneo hilo kuelekea Wilaya ya Kilwa Masoko.

Mgombea Mwenza Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Rufiji kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dk. Seif Rashid, wakati wa mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Muhoro, Tarafa na Kata ya Muhoro, Wilaya ya Rufiji mkoa wa wa Pwani, leo mchana.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.