*Donge yaongoza kwa kura ya ‘Hapana’ Kura ya Maoni
WANANCHI wa Zanzibar waliokusanyika kwenye ukumbi wa Bwawani kwa ajili ya kusikiliza matokeo ya kura za maoni zilizopigwa na wananchi juzi, walifurahia matokeo ya ushindi baada ya kutangazwa matokeo hayo na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Khatib K. Mwinyichande.
Mwenyekiti huyo alitangaza kuwa Waliopiga kura ya ndiyo wameshinda kwa aslimia 66.4 dhidi ya waliopiga kura ya hapana na kuwafanya wananchi waliokuwamo ukumbini humo kurukaruka kwa furaha huku wakipiga vigeregere na makofi na kumshangilia Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Hamadi, aliyekuwamo ukumbini humo akifuatilia matokeo hayo.
Aidha Mwenyekiti huyo alitangaza kuwa jumla ya watu waliojiandikisha kupiga kura walikuwa ni 293, 039 na kura halali zilikuwa ni 284, 318, huku kura zilizoharibika zikiwa ni 8,721 na kuongozwa na kura za ndiyo ambazo zilikuwa ni 188,705 na kura za hapana zikichukua nafasi ya mwisho ambapo zilipatikana jumla ya kura za hapana, 95, 613.
Kwa hatua hiyo ya matokeo hayo ya uchaguzi wa kura ya maoni iliyopigwa Julai 31 mjini Zanzibar, imeonyesha dhahili kuwa wananchi wa Visiwani humo wamekubaliana na kulipokea kwa mikono miwili suala zima la uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Hata hivyo katika uchaguzi huo ni Jimbo la Donge pekee ndilo lililoonekana kuwa na kura nyingi za HAPANA, ambapo katika kura hizo za ndiyo zilikuwa ni 1,266 sawa na asilimi 28.6, huku za hapana zikiwa ni 3234 sawa na asilimia 71.4
Katika hafla hiyo ya kutangaza matokeo kwa upande wa Chama cha CUF kiliwakilishwa na Katibu Mkuu, Maalim Seif Hamad na kwa upande wa CCM, alikuwapo Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Saleh Ramadhan Feruz, huku ukumbini humo wakionekana wanachama wengi wa Cuf kuliko CCM.
Mwenyeiki wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar aliishukuru Serikali kwa kuweza kutimiza wajibu wa kufanikisha suala hilo muhimu kwa wananchi wa Zanzibar na Taifa kwa ujumla, na kuwashukuru wananchi wote kwa ujumla kwa kujitokeza kupiga kura hiyo ya maoni kwa amani na utulivu na kuwataka kuwa na moyo huo hadi katika Uchaguzi mkuu ujao unaotarajia kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Saleh Ramadhan Feruzi na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakifurahia ushindi wa kura ya ndiyo baada ya matokeo.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akipongezwa na Mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Siasa kutoka Ubalozi wa Uingereza, Mark Polatajko, baada ya kutangazwa matokeo ya Uchaguzi wa kura ya Maoni kwenye Ukumbi wa Bwawani mjini Zanzibar.

Wanachama wa CCM na CUF wakishangilia ushindi huo katika mitaa ya mjini Zanzibar baada ya kutangaza matokeo.
sebene la dufu mitaani........
sebene la dufu mitaani........
No comments:
Post a Comment